Maiti walioopolewa Mererani sasa wafikia 35

Idadi ya maiti waliopolewa kutoka migodi ya tanzanite huko Mererani imefikia 35 baada ya wengine saba kuopolewa jana usiku.

Na Radio One Habari



Idadi ya maiti waliopolewa kutoka migodi ya tanzanite huko Mererani imefikia 35 baada ya wengine saba kuopolewa jana usiku.


 


Habari hizo zinasema maiti hao saba wameopolewa kutoka mgodi wa Roita.


 


Pamoja na kuendelea kuwatafuta maiti wengine kutoka migodi hiyo, kazi inayofanyika sasa ni kuziba eneo lililobomolewa na kujenga mifereji ya kuongoza maji kutoka maeneo ya mafuriko, kazi ambayo inafanywa na vikundi mbalimbali wakishirikiana na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.


 


Habari zaidi kutoka eneo la tukio zinasema wawakilishi wa Benki ya National Micro Finance wako eneo hilo kukabidhi msaada wa shilingi milioni kumi ili kusaidia kazi hiyo.


 


Aidha, viongozi mbalimbali wa serikali wakiwemo Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mheshimiwa Adam Malima, Mkuu wa Mkoa Manyara, Bwana Henry Shekifu Kamanda anayeongozi operesheni hiyo, Naibu Kamishna wa Polisi Venance Tossi.


 


Source: RADIO ONE

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents