Habari

Makampuni mengine 28 ya China kuwekewa vikwazo na Marekani 

Marekani imesema itayaweka kwenye orodha mbaya makampuni 28 ya China kwa madai ya kukiuka haki za binadaamu na kuwanyanyasa watu wa kabila la Uighur na jamii nyingine za wachache ambazo wengi wao ni Waislamu kwenye jimbo la Xinjiang.

US Commerce Secretary Wilbur Ross

Waziri wa viwanda wa Marekani, Wilbur Ross

Waziri wa viwanda, Wilbur Ross amesema wakati akitangaza hatua hiyo kwamba Marekani haitavumilia ukatili na ukandamizaji wa jamii za walio wachache nchini China.

Kwa mujibu wa Deutsche Welle, Miongoni mwa mashirika 28 yaliyoorodheshwa ni pamoja na ofisi 18 za usalama zilizoko Xinjiang, chuo kimoja cha polisi na kampuni nane za kibiashara pamoja na kampuni zinazoshughulika na vifaa vya ujasusi na utambuzi wa sura ya mtu.

Marufuku hiyo imetangazwa huku kukiwa na mvutano kati ya Marekani na China hasa kuhusu sera ya biashara na vitendo vinavyofanywa na China kwenye jimbo la magharibi la Xinjiang. Hata hivyo Marekani imekanusha kuwa hatua hiyo inahusiana na mazungumzo ya biashara yaliyopangwa kuanza tena wiki ijayo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents