Michezo

Mmiliki wa Manchester United, Malcom Glazer afariki dunia

Mmiliki wa Manchester United Mmarekani Malcom Glazer amefariki dunia jana (May 28) akiwa na umri wa miaka 85.
.
,
Malcom Glazer

Glazer ambae alianza kuugua kiharusi tangu mwaka wa 2006, amewawachia wanae sita umiliki wa klabu hiyo ya Uingereza.

Familia ya Glazer ilinunua United kwa gharama ya Euro milioni 790 mnamo mwezi Mei mwaka wa 2005 licha ya pingamizi kali kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo.

Hata hivyo, Chini ya umiliki wake uliosabibisha deni kubwa kwa klabu hiyo ‘the Red Devils’ walishinda taji la premier ya Uingereza mara tano pamoja na taji la klabu bingwa mwaka wa 2008.

Watoto wa Glazer waliozaliwa Marekani Byan, Joel, na Avram wote wamejumuishwa katika bodi ya klabu hiyo, huku Joel na Avram wakiwa wenyekiti wenza.

Kifo cha Glazer hakitarajiwi kuathiri umiliki wa United, kwani familia hiyo bado inamiliki asilimia 90 za hisa za klabu hiyo huku asilimia 10 inayosalia inamilikiwa na wenyehisa katika soko la hisa la NY stock Exchange.

Glazer alikuwa pia mmiliki wa Tampa Bay Buccaneers iliyobadili sura ya kandanda la Marekani kwa kushinda taji la Super Bowl .

Glazer hakuwahi kukanyaga uwanja wa Old Trafford kutokana na hofu ya kuwaudhi mashabiki wa timu hiyo, ambao walikuwa wanamshutumu kwa kupanga njama ya kuinunua klabu hiyo kwa kutumia madeni.

Source:BBCu

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents