HabariUncategorized

Mambo mawili kuhusu wananchi kubambikiziwa bili za maji

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Isack Kamwele amekiri kuwepo kwa tatizo la wananchi kubambikiziwa bili za maji hata kama hayatoki na kuwahakikishia wabunge kuwa tatizo hilo wameshaliona na wanalishughulikia na mwisho kulimaliza kabisa.

Mh. Kamwele ameyasema hayo leo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama alilohoji

Mamlaka ya Maji imekuwa na tabia ya kuwalimbikizia wananchi bili za maji, Je ni lini serikali itahakikisha inasimamia kidete bili zinazokwenda kwa wananchi zinatokana na bili za maji?

“Ni kweli mamlaka za maji mijini kuna hiyo hali ya kwamba unaletewa bili hata kama maji yalikuwa hayatoki hata Muheshimiwa Rais juzi ameizungumzia hii lakini hili tumeshaliona katika mambo mawili ambayo tumeyagundua moja kuna kitu wanaita service charge unakuwa kwamba wewe umekodi ile mita kwa maana ya kuikodi walikuwa wameweka utaratibu kwamba hata kama maji hayajatoka kwasababu umekodi wanakuchaji .Waziri amewaita wakurugenzi wote na kuwaagiza kurekebisha hili kwa maana ya kuitoa kwasababu siwezi nikakodi kifaa sipati huduma lakini naendelea kukilipia kwa kuwa nyumbani kwangu kwahiyo muheshimiwa mbunge suala hili tumeanza kulifanyia kazi,” alisema Kamwele.

“Lakini lipo tatizo la pili nimlifanyia study kupitia Mamlaka ya Maji Dawasco hawa wahudumu wetu system yetu ya kusoma mita unasoma alafu unakwenda ku-Punch kwenye kompyuta unaweza ukakuta unit 15 ukaona 15 badae ukarudia tena bado inajidabo ndio maana bili zinakuwa kubwa kwahiyo hili nalo tunaliangalia kitaalam ili hiyo dabo isitokeze.Kwahiyo wabunge ni wahakikishie kwamba hili suala tumeshaliona tunalishunghulikia na tutalimaliza.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents