Michezo

Ujio wa Everton TZ si wakitoto: Kuzinufaisha sekta mbalimbali nchini

Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji kutoka SportPesa Tanzania, Abbas Talimba

Ujio wa klabu ya Everton nchini Tanzania inayoshiriki ligi kuu ya nchini Uingereza ni neema kwa tasnia ya michezo pamoja uchumi wa nchi.

Timu hiyo itaingia nchini Julai 12 kwaajili ya kucheza mchezo wake wa kirafiki dhidi ya timu ya Gor Mahia ya Kenya ambayo ni mshindi ya SportPesa Super Cup 2017.

Everton itatua nchini ikiwa na kikosi chake kamili wakiwemo wachezaji wapya iliyowasajili hivi karibuni ambao atapata fursa ya kucheza mechi yao ya kwanza nchini Tanzania.

Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji kutoka SportPesa Tanzania, Abbas Talimba alisema kuwa licha ya mashabiki wa michezo nchini kusubiria kushuhudia mechi hiyo kwa hamu, lakini pia ujio wa klabu hiyo utainufaisha Tanzania katika nyanja mbalimbali ikiwemo za michezo pamoja na utalii.

“Tumeamua kuileta timu ya Everton kucheza katika uwanja wa nyumbani ili kuweza kuitangaza Tanzania kisoka tukiwa na lengo la kuinua vipaji na kuhamasisha wanasoka kuwa makini na kuwekeza katika vipaji vyao ikiwa ni katika harakati za kuinua na kuendeleza soka nchini,” alisema Talimba.

Talimba alisema ujio huo utalinufaisha soka la Tanzania kwani kutakuwa training mbalimbali ambazo zitatolewa na Everton.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents