Michezo

Manchester United yaipa kipigo kikali Swansea

Klabu ya Manchester United imechomoza na ushindi mnono wa magoli 4-0 dhidi ya Swansea mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza .


Magoli ya United yakifungwa na E Bailly dakika ya 45 wakati magoli mengine matatu yakitiwa wavuni na Romelu Lukaku dakika ya 80, Paul Pogba dakika ya 82 huku, Anthony Martial akihitimisha karamu ya magoli dakika ya 84 ya mchezo huo.
Vijana hao wa Jose Mourinho wameonekana kuwafiti zaidi katika kipindi cha pili cha mchezo huo.

Wachezaji wa vikosi vyote viwili ni kama wafuatao
Kwa upande wa Swansea: Fabianski (6), Mawson (5), Olsson (6), Naughton (5), Bartley (6), Fernandez (5), Carroll (6), Fer (5), Mesa (5), Ayew (5), Abraham (6).
Waliyokuwa benchi ni Narsingh (4), Routledge (4), McBurnie (4).

Wakati wachezaji Man Utd ni De Gea (7), Bailly (8), Jones (7), Blind (7), Valencia (7), Matic (7), Mkhitaryan (8), Pogba (7), Mata (7), Rashford (7), Lukaku (7).
Huku waliyokuwa benchi ni Martial (7), Herrera (4), Fellaini (4).

Katika mchezo huo mchezaji, Henrikh Mkhitaryan ndiye aliyeibuka nyota wa mchezo.

Mchezaji, Henrikh Mkhitaryan

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents