Habari

MAREKANI: Mama amuhurumia mumewe mahakamani, licha ya kumuulia watoto wake baba huyo amuombea asipewe hukumu ya kifo 

Mama mmoja wa watoto watano waliouawa na baba yao amelitaka jopo linalosikiza kesi ya mumewe kutomwekea hukumu ya kifo. Amber Kyzer aliambia mahakama moja huko Carolina ya kusini kwamba Tim Jones Jr hakuwaonea huruma wanangu kwa njia yoyote ile lakini wanangu walimpenda sana.

Image result for Amber Kyzer in court

Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 37 alihukumiwa mwezi Mei kwa kuwauawa watoto wake wenye umri kati ya mmoja hadi nane nyumbani kwake karibu na Lexington mnamo tarehe 29 Agosti 2014.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Jopo hilo linajadiliana iwapo Jones anafaa kupewa kifungo cha maisha ama kunyongwa. ”Nasikia kile ambacho watoto wangu walipitia”, alisema bi Kyzer katika mahakama siku ya Jumanne.

”Na kama mama iwapo ningekuwa na uwezo wa kuupasua uso wake ningeupasua. Hicho ndio nilicho nacho ndani yangu”.

Timothy Ray Jones awasilishwa mahakamani

Bi Kyzer aliambia jopo hilo kwamba alikuwa akipinga hukumu ya kifo kwa kipindi chote cha miasha yake

Alisema kwamba licha ya kutamani sheria ‘imkarange’ mumewe asingepenedelea kumchangulia hukumu ya kifo.

”Hakuwaonyesha watoto wangu huruma yoyote” , alisema. ”Lakini watoto wangu walimpenda na iwapo ninazungumza kwa niaba ya yangu na watoto wangu basi hilo ndio tamko langu”.

Bi Kyzer hatahivyo alisema kwamba ataheshimu chochote kitakachotolewa na jopo hilo la majaji.

Alikuwa ameitwa kutoa ushahidi wake na mawakili wa mumewe.

Wanandoa hao walifunga ndoa wiki sita baada ya kukutana 2004 wakati wote walipokuwa wakifanya kazi katika bustani ya watoto ya kucheza katika eneo la Chicago

Watoto wote watano waliuawa na baba yao

Lakini alitoa ushahidi mwezi Mei kwamba ndoa yao ilikuwa imekumbwa na mushkil kwa kuwa alikuwa na masharti mengi na kwamba ‘wanawake hawakutakiwa kusikika bali kuonekana pekee’.

Walipotengana baada ya miaka tisa alimpatia watoto aishi nao kwa sababu alikuwa akifanya kazi iliokuwa ikimpatia pato la $80,000(£63,000) kwa mwaka.

Mwanamke huyo alikuwa akiwaona watoto hao kila Jumamosi katika mkahawa mmoja.

Siku ambayo Jones aliwaua watoto hao , mahakama iliambiwa kwamba alikasirika alipomuona mtoto mwenye umri wa miaka sita Nahtan akicheza na plagi ya umeme nyumbani.

Alimuua mvulana huyo na baadaye kuwanyonga watoto wengine wanne-Elaine, Gabriel, Elias na Mera.

Jones baadaye aliifunga miili yao katika mfuko wa plastiki, jopo hiyo liliambiwa na kuiweka ndani ya gari moja na kuondoka kwa siku tisa kabla ya kuwacha mabaki hayo katika jimbo la Alabama.

Alikamatwa katika kituo kimoja cha traffiki mjini Missisipi wakati maafisa wa polisi walipotambua harufu iliokuwa ikitoka ndani ya gari hilo.

Jones alikana kwamba alihusika na mauaji ya watoto hao alipowasilishwa mahakamani.

Upande wa mshukiwa ulisema kwamba alikuwa akiugua ugonjwa wa kiakili ambao pia ulimuathiri mamake.

Wanasema kuwa aliathirika baada ya mkewe akumtoroka na kuanza uhusiano na kijana mmoja jirani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents