Habari

Marekani yatuma mfumo wa kukinga makombora na meli ya kijeshi mashariki ya kati huku wasiwasi kati yake na Iran ukiendelea

Marekani inatuma mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora na meli ya kivita katika eneo la mashariki kutokana na hali ya waiswasi iliopo katiya taifa hilo lna Iran.

The Nimitz-class aircraft carrier USS Abraham Lincoln transits the Strait of Gibraltar, entering the Mediterranean Sea as it continues operations in the 6th Fleet area of responsibility, April 13, 2019.

Meli hiyo ya kivita ya USS Arlington, inayosafirisha magari na ndege , itajiunga na kundi la kijeshi la USS Abraham Lincoln katika ghuba , maafisa wamesema.

Makombora ya US B-52 bombers pia yamewasili katika kambi moja nchini Qatar, idara hiyo imesema. Imesema kuwa hatua hiyo inafuatia vitisho vya operesheni za vikosi vya kijeshi vya Marekani katika eneo hilo.

Marekani imetoa habari chache kuhusu uwezo wa tishio hilo, ambao Iran umepinga kama ujinga, ikitaja hatua hiyo ya Marekani kama vita vya kiakili vyenye lengo la kuitishia nchi hiyo.

Wakati huohuo chombo cha habari cha Isna News Agency kilimnukuu kiongozi mmoja mkuu wa dini , Yousef Tabatabai-Nejad akisema kuwa ”msafara huo wa Marekani unaweza kuharibiwa na kombora moja pekee”.

Je Marekani imesema nini?

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Siku ya Ijumaa idara ya Pentagon ilisema kuwa Marekani haitaki vita na Iran lakini Washington iko tayari kulinda vikosi vya Marekani na mali zake katika eneo hilo.

”Idara ya ulinzi inaendelea kufuatilia kwa karibu vitendo vya utawala wa Iran”, ilisema katika taarifa.

Iliongezea kuwa mfumo huo wa makombora ambao unaweza kutungua makombora ya masafa marefu na yale ya chini chini na ndege za kijeshi pia utapelekwa katika eneo hilo iwapo kuna uwezekano wa shambulio lolote.

Mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora kutoka Marekani

Mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora kutoka MarekaniĀ 

Maafisa wameambia vyombo vua habari vya nchini Marekani kwamba meli hiyo ya USS Arlington ilitarajiwa kuwasili katika eneo hilo lakini imepelekwa katika eneo hilo mapema ili kutoa uwezo wa amri zitakazotolewa na udhibiti.

Siku ya Jumapili , mshauri wa maswala ya usalama nchini ,Marekani John Bolton alisema kuwa kupelekwa kwa vifaa hivyo vya kijeshi kutatoa ujumbe wa wazi kwa utawala wa Iran kwamba shambulio lolote dhidi ya mali ya Marekani katika eneo hilo litajibiwa na uwezo mkubwa wa kijeshi.

Meli hiyo ya USS Abraham Lincoln ilipita kupitia rasi ya Suez siku ya Alhamisi , kulingana na idara ya ulinzi nchini Marekani.

Mwandishi wa BBC anayeshughulikia maswala ya Ulinzi na diplomasia Jonathan Marcus anasema kuwa huku ikiwa sio jambo la kawaida kwa meli ya kubeba ndege kutumwa katika Ghuba , hatua hiyo itasababisha hofu ya uwezekano wa vita kuebuka kwa ajali ama mipango.

Je hali ya uhusiano wa Iran na Marekani iko vipi?

Mwaka uliopita , rais wa Marekani Donald Trump alijiondoa katika mkataba wa kinyuklia wa Iran ambao Marekani na mataifa mengine yalikuwa yameingia makubaliano na Iran 2015.

Katika makubaliano hayo , Iran ilikuwa imekubali kupunguza vitendo vyake vya utumizi wa nyuklia na badala yake kuruhusu wachunguzi wa kimataifa kuingia nchini humo kukagua ili waondolewe vikwazo.

Na mwezi uliopita Ikulu ya Whitehouse ilisema kuwa ingeyaondolea msamaha mataifa matano ikiwemo- China, India, Japan, Korea Kusini na Uturuki ambayo yalikuwa yakiendelea kununua mafuta ya Iran.

https://www.voanews.com/a/us-sending-more-military-power-to-counter-iranian-threat/4913180.html

Wakati huohuo Marekani pia imeliorodhesha jeshi la Iran kuwa kundi la kigaidi.

Utawala wa rais Trump unatumai kuishinikiza Iran kuanzisha mazungumzo ya mkubaliano mapya ambayo yatasimamia sio tu vitendo vyao vya kinyuklia bali pia mipango yake ya uundaji wa makombora ya masafa marefu mbali na kile maafisa wanasema ni tabia yake ya ukandamizaji katika eneo lote la mashariki ya kati.

Vikwazo hivyo vimesababisha kushuka kwa uchumi wa Iran , vikisukuma thamani ya sarafu yake chini mbali na kuwafukuza wawekezaji wa kigeni na kusababisha maandamano.

Iran imetishia kulipiza kisasi kwa kufunga mlango wa Hormuz ambapo mafuta mengi yanayotumika duniani hupitia.

Awali Iran wiki hii ilitangaza kwamba imesitisha utekelezwaji wa sheria 2 za makubaliano ya 2015 kutokana na vikwazo ambavyo vimewekwa na Marekani.

Pia ilitishia kuanzisha upya mpango wa kutengeneza madini ya Uranium iwapo vikwazo hivyo vitaendelea katika siku 60 zijazo.

Mataifa yenye uwezo mkubwa barani Ulaya yamesema kuwa yataendelea kuheshimu makubaliano hayo ya Iran lakini yatakaa masharti yoyote ya utawala huo wa Tehran ili kuyalinda.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents