Michezo

Mashabiki Msikate Tamaa – Yusuph Manji

Mwenyekiti wa klabu ya Dar Young Africans, Yanga, Bw.Yusuph Manji, amewataka mashabiki wa timu hiyo kutosononeka sana kwa kipigo cha mabao 4-0 yaliyosababisha kutolewa kwenye michuano ya kimataifa Na MC Algeria.

Bw. Manji akiongea na mtandao wa Goal, amesema, anachotaka ni kuhakikisha timu hiyo inapambana kutafuta nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa mwakani kwa kubeba taji la ligi kuu ya Vodacom au ubingwa wa kombe la FA.

“Niliongea na timu yetu kabla ya kwenda Algeria na niwahakikishie mashabiki wetu wasikate tamaa. Ni kweli tumetolewa lakini tuendelee kuipa support timu yetu ili iweze kupata nafasi nyingine ya michuano ya kimataifa. Nataka kuisuka upya Yanga ili iwe na uwezo wa kucheza mashindano makubwa Afrika na kufika mbali,” amesema Manji.

Kiongozi huyo amesema kilichosababisha timu yake kuyumba ni matatizo aliyoyapata, na ingawa bado hayajamalizika, anaamini yatakaa sawa huku lengo lake la kukiimarisha kikosi hicho kutimia,kwa kumruhusu kocha Lwandamina kusajili mchezaji anayemuhitaji

Amesema hilo kwake halina tatizo isipokuwa amemtaka kila mmoja kutimiza majukumu yake ndani ya timu na kulifikisha pale walipokusudia ingawa wamekumbwa na matatizo ya ya mishahara kwa kipindi hiki cha matatizo.

Amesema Yanga ni timu kubwa Afrika na kama Mwenyekiti hatakubali kuwaona wanaadhirika kwa kushuka chini kimafanikio, ndio maana anataka kurudisha ubora wa timu ili kufikia kile walichokikusudia msimu huu.

Kipigo cha 4-0 kimeifanya Yanga kutolewa kwenye michuano ya Kombe la shirikisho Afrika, kwa jumla ya mabao 4-1 na sasa inarejea nyumbani.

Source: goal.com

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents