DStv Inogilee!

Matokeo ya mechi za kombe la dunia la Vijana U20

Michuano ya kombe la dunia la vijana chini ya umri wa miaka 20 inaendelea kushika kasi huko nchini Korea ya kusini ikiwa katika ngazi ya makundi.


Wachezaji wa kikosi cha Zambia wakishangilia baada ya ushindi dhidi ya Iran

Katika michezo ya kundi C wawakilishi wa Afrika timu ya Zambia walipata ushindi mabao 4-2 dhidi ya timu ya Iran. Nao Costa Rica wakatoshana nguvu na Ureno kwa Sare ya bao 1-1.
Kwenye kundi D Afrika ya kusini walichapwa na Italia kwa mabao 2-0, huku Uruguay wakiwafunga Japani kwa 2-0.


Kikosi cha timu ya Taifa ya Uruguay

Michuano hiyo inaendelea tena leo katika kundi E Ufaransa watacheza na Vietnam, na New Zealand wakipepetana na Honduras.
Katika kundi F Ecuador wataonyesha ubavu na Saudi Arabia, huku Senegal wakicheza na Marekani.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW