Michezo

Matokeo ya Mechi za robo fainali ya michuano ya klabu Bingwa Barani Ulaya iliyochezwa usiku wa April 5 2016

Michezo ya robo fainali ya michuano ya klabu Bingwa Barani Ulaya ilichezwa usiku wa April 5 2016 katika viwanja vya Nou Camp ulizikutanisha timu za FC Barcelona dhidi ya Atletico Madrid na katika uwanja wa Alianz Arena ulichezwa mchezo wa FC Bayern dhidi ya Benfica.

Torres

Luis Suarez amepiga bao mbili Barcelona ikitoka nyuma na kuichapa Atletico Madrid 2-1 ikiwa na watu 10 uwanjani kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Champions League.

article-3525055-32E08D7D00000578-866_636x368

Atletico ilifanikiwa kupata goli muhimu la ugenini wakati Fernando Torres alipofanya kazi ya ziada kupachika bao hilo kipindi cha kwanza cha mchezo huo.

Baade Torres alitolewa nje kabla ya half-time baada ya kuonesha kadi mbili za njano ndani ya dakika saba.

Nao Bayern Munich walishinda goli moja dhidi ya Benfica ya Ureno, goli likifungwa na Arturo Vidal.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents