Habari

Mauaji ya Jamal Khashoggi: Mwanamfalme wa Saudia kuchunguzwa

Kuna ushahidi kamili kwamba mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman na maafisa wengine wa ngazi za juu wanahusika binafsi kwa muaji ya Jamal Khashoggi, kulingana na mtaalamu wa Umoja wa mataifa.

Jamal Khashoggi (kushoto) na Mohammed bin Salman (R)

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Ripoti ya mtaalamu huyo wa UN Agnes Callamard inasema kuwa ushahidi huo unahitaji kufanyiwa uchunguzi na jopo huru la kimataifa lisilo pendelea upande wowote. Khashoggi aliuawa katika ubaloizi wa Saudia mjini Instanbul na maajenti wa Saudia.

Watawala wa Saudia wanasisitiza kuwa wauaji wake hawakutumwa na mwanamfalme Mohammed. Ufalme huo wa Ghuba umeweka washukiwa 11 wasiojulikana katika jopo kujibu mashtaka na tayari imewawekea hukumu ya kifo watano kati yao.

Hatahivyo Bi Callamard alisema kuwa jopo hilo lilishindwa kuafikia viwango vya kimataifa na kulitaka kuvunjiliwa mbali.

Je Jamal Khashoggi aliuawa vipi?

Mwandishi huyo aliyekuwa na umri wa miaka 58 , na aliyekuwa akiandikia gazeti la the Washington Post na mkosoaji mkubwa wa mwanamfalme Mohammed mara ya mwisho alionekana akiingia katika ubalozi wa Saudia tarehe 2 Oktoba ili kuchukua nakala alizohitaji ili kumuoa mchumba wake Hatice Cengiz.

Bi Callamard , mtaalamu huyo wa Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji ya kiholela alisema kuwa Khashoggi aliuawa kikatili ndani ya ubalozi huo.

Jamal Khashoggi: What we know about the journalist’s disappearance and death

Naibu wa mwendesha mashtaka wa Saudia Shalaan Shalaan aliambia maripota kwamba mnamo mwezi Novemba kwamba mauaji hayo yaliagizwa na kiongozi wa wapatanishi aliyetumwa mjini Instanbul na naibu afisa mkuu wa ujaususi ili kumlazimisha Khashoggi kurudi katika ufalme huo kutoka mafichoni kwake.

Wachunguzi waliamua kwamba Khashoggi alilshikwa kwa nguvu baada ya kukataa na kudungwa sindano iliokuwa na kiwango cha juu cha dawa hatua iliosababisha kifo chake”, alisema bi Shaalan .

”Mwili wake baadaye ulikatwakatwa na kupatiwa mshirika wa ajenti hao nje ya ubalozi” , aliongezea.

Watu watano tayari wamekiri kumuua, bi Shaalan alisema akiongezea ” mwanamfalme hakuwa na habari kuhusu hatua hiyo”.

Ripoti hiyo inasema nini?

Mnamo mwezi Januari afisi ya haki za kibinaadamu katika Umoja wa Mataifa ulimpatia bi Callamard jukumu la kuchunguza kuhusu kiwango cha utaifa na watu binafsi waliohusika katika mauaji hayo.

Maafisa waandamizi wa Saudia wanasisitiza kuwa kifo cha Khashoggi kilitokana na operesheni mbaya , lakini mchunguzi huyo wa UN anasisitiza kuwa ni mauaji ya kiholela ambapo ufalme wa Saudia unadaiwa kuhusika.

Kutokana na sheria ya haki za kibinaadamu, jukumu la serikali sio swali kwa mfano, ni maafisa gani wa serikali waliagiza mauaji ya Khashoggi, iwe mmoja ama zaidi aliagiza kutekwa kwake kabla ya kudaiwa kuwa ajali ama iwapo maafisa hao walitekeleza mauaji hayo kibinafsi.

Bi Callamard pia alisema kuwa kulikuwa na ushahidi uliotaka uchunguzi zaidi kufanywa kuhusu maafisa wa ngazi za juu. Mtaalamu huyo anasema kwamba mwanamfalme huyo anahitaji kuwekewa vikwazo ambavyo tayari vinaaathiri mataifa wanachama ikiwemo Marekani, dhidi ya watu binafsi waliotajwa kuhusika na mauaji hayo.

Amesema kuwa vikwazo hivyo vinafaa kulenga mali yake katika mataifa ya kigeni, hadi pale ushahidi utakapopatikana kwamba hakuhusika na mauaji ya bwana Khashoggi”, alisema.

Kesi ya washukiaw hao 11 inayoendelea nchini Saudia inafaa kusitishwa kulingana na Callamard , kwa kuwa huo ulikuwa uhalifu wa kimataifa ambapo inaweza kuendeshwa mahala popote.

Hatua hiyo itaruhusu mataifa kama vile Uturuki , Marekani kuweza kuwashtaki wauaji wake. Ripoti hiyo inasema kuwa baraza la Umoja wa Mataifa linafaa kufuatilia uchunguzi kuhusu mauaji ya Khashoggi ili kuanzisha kesi kubwa na kutafuta mikakati kwa watu kuchukua jukumu kama vile jopo. Hakujakuwa na tamko lolote kuhusu ripoti hiyo kutoka kwa serikali ya Saudia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents