Habari

Mbwa Kuno kukabidhiwa Medali kwa kuwaokoa Wanajeshi mbele ya risasi kali

Mbwa wa jeshi aliyekimbia na bila kuogopa risasi zilizokuwa zikifyatuliwa na adui ili kuokoa maisha ya wanajeshi wa Uingereza waliokuwa wakipigana na al-Qaeda nchini Afghanistan anatarajiwa kutuzwa tuzo ya juu zaidi ya wanyama.

Kuno: Military dog to receive UK's highest honour for animals after he was injured tackling al-Qaeda gunman | The Independent | Independent

Wakati wa uvamizi, mbwa huyo aina ya Malinois kutoka Ubelgiji kwa Jina Kuno alimkabili mpiganaji mmoja aliyekuwa na bunduki na alipigwa risasi katika miguu yake yote miwili.

Baada ya kupoteza mguu wake mmoja kutokana na shambulio hilo la risasi , alikuwa mbwa wa kwanza wa Uingereza kuwekwa miguu bandia.

Mbwa huyo mwenye umri wa miaka minne atapokea medali yake ya Dickin kutoka kwa shirika la hisani linaloshughulikia wanyama wagonjwa PDSA.

Akiwa mwanajeshi mstaafu na kupelekwa nyumbani Uingereza, Kuno ambaye alifunzwa kufichua vilipuzi , silaha na kuwakabili maadui atatuzwa medali hiyo katika sherehe mwezi Novemba.

Kuno na wamiliki wake walikuwa wamepelekwa nchini Afghanistan kusaidia vikosi maalum wakati wa shambulio la usiku lililokuwa likiwalenga wapiganaji wa al-Qaeda mwaka uliopita wakati walipovamiwa.

Kikosi hicho kilichoshambuliwa kwa maguruneti na risasi kali kutoka kwa adui kilishindwa kusonga mbele. Kuno alitumwa kukabiliana na adui.

Na bila kusita alikimbia katikati ya risasi kali akiwa amevalia miwani ya kuona usiku ili kumkabilia mpiganaji aliyekuwa akitekeleza mashambulio hayo, na kumuangusha chini hatua iliozuia mashambulio zaidi.

Ni hatua hiyo ya Kuno iliobadili hali hiyo na kuvisadia vikosi vya Uingereza kukamilisha lengo lao kwa ufanisi mkubwa.

Lakini wakati alipokuwa akimkabili mshambuliaji huyo alipigwa risasi miguu yake yote ya nyuma na kutibiwa na wamiliki wake ndani ya helikopta wakati walipokuwa wakielekea eneo lililo salama.

Alipata majeraha kadhaa – ikiwemo risasi ilioukosa mshipa muhimu wa damu na kumfanya kuhitaji upasuaji wa dharura wa kuokoa maisha yake kabla ya kurudishwa nyumbani Uingereza kwa matibabu zaidi.

Madaktari wa mifugo walilazimika kumkata miguu yote miwili ya nyuma ili kuzuia maambukizi ambayo yangehatarisha maisha yake.

Baada ya kurudi Uingereza kupitia ndege ya kijeshi alifanyiwa upasuji mkubwa.

Kama wanajeshi waliojeruhiwa , Kuno alianza mpango wa ukarabati ili kuwezesha neva zake na misuli kufanya kazi kama kawaida na inadaiwa kuwa alifurahia sana mpango wa kumsaidia kutembea upya katika kifaa cha mazoezi kwa jina Treadmill.Kuno akikimbia katika ufuo wa bahari

Ndani ya mwezi mmoja , alikuwa tayari kuvalishwa miguu hiyo bandia ili kuchukua mahala pake miguu yake iliokatwa.

Kuno ambaye alikuwa katika ziara yake ya pili wakati alipojeruhiwa , ni mbwa wa kwanza nchini Uingereza kuvalishwa kifaa hicho, kinachomwezesha kukimbia na kuruka bila tatizo lolote hatua inayompatia miaka mingi katika maisha yake baada ya kustaafu.

Uvamizi huo ulikuwa muhimu zaidi dhidi ya al-Qaeda katika kipindi cha miaka kadhaa.

Waziri wa ulinzi nchini Uingereza Ben Wallace alisema: Bila Kuno , operesheni ingekuwa ngumu sana na ni wazi kwamba aliokoa maisha ya wanajeshi wa Uingereza siku hiyo.

Uvamizi huo ulikuwa mojawapo ya ile muhimu zaidi dhidi ya al-Qaeda katika miaka kadhaa. Hadithi ya Kuno inatukumbusha sio tu uangalizi wa hali ya juu tunaowapatia wanajeshi na mbwa wetu , lakini pia uangalizi wa hali ya juu ambao jeshi la Uingereza linatoa kwa wanyama wanoshirikiana na jeshi hilo.

Kuno atakuwa mbwa wa 72 kupokea tuzo hiyo huku mbwa wengine 34 wakiwa tayari walituzwa , ikiwemo njiwa 32 kutoka kwa vita vya pili vya dunia, farasi wanne na paka mmoja.

Mbwa mwengine wa kijeshi aliyetuzwa ni Conan aliyejeruhiwa wakati wa uvamizi uliomuua kiongozi wa Islamic State Abu Bakr al-Baghdad.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents