Burudani

Mchafuko Intercollege Bash Dodoma

 

Habari za uhakika zilizofikia B5, ni kwamba tamasha la Inter College Bash chini ya uratibu wa Str8 Muzik, lililofanyika Jumamosi na kuhusisha vyuo vikuu Dodoma, lilipata mchafuko baada ya polisi kusambaratisha shughuli hiyo na kupelekea kuwa na fujo uwanjani hapo.

Inasemekana kwamba, Polisi walifika katika eneo hilo wakati Joh Makini alikuwa stejini na kuamrisha muziki kuzimwa kana kwamba muda umekwisha.

Fujo na vurugu lilitokea kwani wanafunzi hao hawakuwa tayari kuliachia burudani lao ambalo ndio kwanza lilikuwa linakolea kuanza.

Mali aina za kamera na vifaa vya muziki viliharibika pamoja na baadhi ya wanafunzi kujeruhiwa kutokana na fujo hizo.

B5 iko kwenye harakati za kuwatafuta waratibu pamoja na msemaji wa polisi ili kukuporomoshea habari kamili.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents