Michezo

Mchezaji ‘The Juice’ aachiwa huru kifungo cha miaka 33

By  | 

O.J. Simpson maarufu kama The Juice ambaye ni mchezaji wa zamani wa soka la Marekani na muigizaji, amesamehewa kifungo chake cha miaka 33 alichohukumiwa.

Jopo linalohusika na msamaha kwa wafungwa limefikia maamuzi hayo kwa The Juice mwenye umri wa miaka 70 ambaye alihukumiwa kifungo hicho katika gereza la Nevada na tayari alishakuwa ametumikia kifungo cha takribani miaka tisa.

Mchezaji huyo alikuwa akishtakiwa kwa makosa yapatayo 10 ambapo kubwa zaidi likiwa la uvamizi wa hoteli ya Las Vegas mwaka 2007. Wakati huo huo mwaka 1995 mzee huyo aliwahi kushtakiwa kwa kosa la mauaji ya aliyekuwa mkewe, Nicole Brown Simpson na rafiki yake Ron Goldman hata hivyo aliachiliwa.

Kwa sasa The Juice ataachiwa huru rasmi ifikapo mwezi Octoba ya mwaka huu.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments