Michezo

Mchezaji wa Tottenham Hotspurs atalii mbuga za wanyama nchini

Siku chache baada ya mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Manchester united, David Beckham kutua nchini Tanzania kwa ajili ya kutalii akiwa na familia yake. Na kuwasili nchini kwa Mfaransa, Mamadou Sakho beki wa Liverpool kwa ajili ya kutalii mkoani Arusha na kutazama namna Tanzania ilivyobarikiwa na maliasili.

Mchezaji wa Tottenham Hotspurs ya Uingereza na  timu ya Taifa ya Denmark Christian Eriksen.

Ujio wa wachezaji hawa ni kama kumezidi kuifungulia milango Tanzania katika sekta ya utalii baada ya safari hii kupata ujio wa Mchezaji wa klabu ya Tottenham Hotspurs ya Uingereza na kiungo wa timu ya Taifa ya Denmark Christian Eriksen.

Mchezaji wa Tottenham Hotspurs ya Uingereza na  timu ya Taifa ya Denmark Christian Eriksen

Mbali ya Christian Eriksen, mchezaji raia wa Kenya na klabu ya Spurs Victor Wanyama naye amewasili nchini kwaajili mapumziko yake.

Mchezaji raia wa Kenya na klabu ya Spurs Victor Wanyama akitua nchini

Christian Eriksen amekuwa tofauti kidogo na mchezaji Mamadou Seakho ambaye alikuwa haoni tabu kuposti picha zake na kuandika kuwa yupo Tanzania

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents