Habari

Meli iliyopata ajali miaka 400 yapatikana, inadaiwa ilikuwa njiani kutoka India

Watafiti wa mambo ya kale wamegundua meli iliyopata ajali miaka 400 iliyopita karibu na pwani ya Ureno, katika tukio ambalo wataalam wameliita “ugunduzi muhimu”.

Kwa mujibu wa mtandao wa REUTERS, baadhi ya viungo, vyombo vya kauri na mizinga ikiwa na nembo ya Ureno vimetapakaa katika eneo la karibu na Cascais ambapo si mbali sana kutoka Mji Mkuu Lisbon.

Image result for Shipwreck discover 400 years past in Cascais
Wagunduzi hao waamini kwamba meli ilikuwa njiani kutoka India wakati ilipozama kati ya mwaka 1575 na 1625. Nyakati hizo zinakadiriwa kuwa ndiyo kilele cha biashara ya viungo kati ya Ureno na nchi za Asia.

Image result for Shipwreck discover 400 years past in Cascais

Inadhaniwa kuwa huu ni ugunduzi mkubwa kabisa ambao umechukua takribani miaka 10 kwa mujibu wa mkurugenzi wa zoezi hilo, Jorge Freire ambapo akisisitiza ni jambo muhimu zaidi kwa Ureno.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents