Burudani

Mesen Selekta aunga mkono kauli ya Master Jay, ‘maprodyuza wengi ni wanafiki’

Prodyuza Mesen Selekta anaonekana kuikubali kauli ya kuwa maprodyuza wengi Bongo ni wanafiki baada ya kushindwa kutekeleza azimio la kutorekodi wimbo chini ya Tsh. 1,000,000 kama ilivyowahi kudai na prodyuza mkongwe Master Jay.

Mesen amesema ni kweli alichoongea Master Jay kwani vikao vya maprodyuza vilikuwepo na walikuwa wanakutana baada ya siku kadhaa na mada ya malipo ilishajadiliwa.

“Sasa unajua kinachokuja kutokea maprodyuza wanaokuja ni wengi, zamani studio zilikuwa chache kwa hiyo umoja wa kufanya maamuzi ulikuwa ni rahisi tofauti na sasa hivi studio ni nyingi, hivyo mtu anaangalia studio yangu ndio inaanza tukianza kurekodi wote milioni moja nitapataje wateja?, kuna muda mwingine mtu anapiga kishikaji,” ameiambia Twenzetu ya Times Fm na kuongeza.

“Ni suala mbalo ni gumu lakini cha msingi ni haki za muziki wa maprodyuza zitendewe haki katika malipo ya nyimbo kila inapotoka prodyuza awe na asilimia yake ya malipo nadhani hiyo pia itasaidia,” amesisitiza.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents