Michezo

Messi, Ronaldo wakutanishwa ‘uso kwa uso’ na UEFA

Washambuliaji wa klabu za Real Madrid na Barcelona, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wamekutanishwa na Shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) kwenye  orodha ya wachezaji watatu wanaowania tuzo ya mchezaji bora barani humo.

Kupitia mtandao wa UEFA jina la tatu kwenye orodha hiyo ni la mlinda mlango wa klabu ya Juventus, Gianluigi Buffon ambaye amekuwa na msimu mzuri uliopita 2016/17 kwa kufanikiwa kutinga fainali ya klabu bingwa barani Ulaya huku akifanikiwa kubeba ndoo ya Serie A na kombe la Coppa Italia.

Mshindi mara tano wa Ballon d’Or, Lionel Messi yeye hakuwa na msimu mzuri ukilinganisha na wenzake kwani msimu uliopita aliambulia taji moja tu la kombe la Mfalme ‘ Copa del Rey’ nchini Hispania.

Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo yeye ndiye anayepewa asilimia kubwa kuchukua tuzo ya mchezaji bora barani Ulaya kutokana na kuisaidia klabu yake kuchukua ndoo ya Ligi kuu nchini Hispania na kombe la klabu bingwa barani Ulaya kwenye fainali ambayo Madrid waliichapa Juventus goli 4-1, huku mshambuliaji huyo akitupia magoli mawili.

Wachezaji wengine walioingia kwenye orodha ya wachezaji kumi bora kuanzia nafasi ya nne ni Luka Modrić (Real Madrid), Toni Kroos (Real Madrid), Paulo Dybala (Juventus), Sergio Ramos (Spain, Real Madrid), Kylian Mbappé (Monaco), Robert Lewandowski (Bayern München) na Zlatan Ibrahimović (Manchester United).

Tuzo hizo zitatolewa siku ya Alhamisi ya tarehe 24 Agosti mwaka huu siku ambayo droo ya makundi ya klabu bingwa barani Ulaya itachezeshwa.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents