Burudani

Mfahamu zaidi Christine ‘Seven’ Mosha, meneja wa Alikiba

Kuna uwezekano ya kuwa wengi hawamufahamu Seven Mosha kama vile wanavyofahamika wasanii anaowasimamia kazi zao za muziki.

Seven Mosha akiwa na Alikiba

Jumapili, Feb 5, 2017 akiongea na kitengo cha Buzz kwenye gazeti kuu nchini Kenya la Nation, Mosha alieleza kuwa alikuwa mtangazaji katika kituo cha redio cha Clouds FM na pia kituo hicho kilipoanzisha label ya kurekodi maarufu kama Smooth Vibe, alikuwa mhusika mkuu katika masuala ya kusikiliza na kuandika muziki.

Alitoka Clouds FM mwaka wa 2009 na akajiunga na kituo cha televisheni cha MTV ambapo anasema alihudumu kwa takribani miaka mitano toka 2005-2010 ambapo alikuwa katika kitengo cha ( Artiste and Repertoire) maarufu kama A&R. Pia Seven alihudumu katika kampuni kubwa ya muziki duniani ya Sony kwa muda kabla ya kusimamia tawi la Rockstar4000.

Seven Mosha anasema alizaliwa Nairobi Kenya lakini akahamia Moshi, Tanzania. Familia yake ambayo iliishi katika mtaa wa kifahari wa Lavington jijini Nairobi, ilihamia Tanzania akiwa na umri wa miaka minne tu. Jina lake la kuzaliwa ni Christine Mosha lakini baada ya kufundishwa kuhusu maajabu saba ya ulimwengu na dhambi saba kuu katika dunia basi nambari saba ”Seven” ikawa nambari yenye nguvu katika maisha yake na ndio maana akajiita Seven kama aka yake.

Aliliambia gazeti hilo kuwa, haamini kama anaitwa Christine, maana kama angalikuwa na chembechembe za hulka la jina Christine, marafiki zake wangelikuwa Elizabeth ama Victoria ambao wengi wao huwa wanategemea mabwana zao kuwafanyia kila kitu katika maisha ilhali wakibaki kufanya kazi za nyumbani kwa kimombo ”Housewives.”. Ni kilinukuu gazeti hilo, (She does not believe she is a Christine,if she had a Christine character her friends would be called Elizabeth or Victoria and she would a housewife and stay at home).

Akigusia ushindani uliopo kati ya Diamond na Alikiba, Mosha aliliambia gazeti hilo kuwa, anaamini ushindani katika tasnia ya burudani ya muziki ni mzuri, kwasababu inawapa wasanii motisha ya kuvalia njuga kazi zao na kutoa vitu venye ubora wa hali ya juu na kuuikuza sanaa ya Afrika Mashariki katika viwango vya dunia.

Lakini akaongezea kuwa ataunga mkono ushindani kama huo pekee, pale ambapo hautahatarisha maisha ya masanii yeyote yule. Bali anafurahia vile Diamond na Alikiba wanavyoshinda kutoka production ya muziki hadi kwa style za kimaisha.

Mosha aliongezea kuwa, huu ni mwaka wake wa sita tangu aanze kufanya kazi na Alikiba. Na walikutana kwa mara ya kwanza katika project ya One8 ambapo katika project hiyo aliwasimamia wasanii wa Afrika Mashariki na alisisitiza kuwa alipenda kila kitu kuhusu Alikiba. Baada ya project ya One8 kuisha walikuwa wakiwasiliana na mwisho wakaamua kufanya kazi pamoja. Pia Seven ni rafiki mkubwa wa Lady Jaydee, na picha ya macho yake ndio yalikuwa kwenye cover ya album ya kwanza ya Lady Jaydee ”Machozi”.

Mkali wa Yahaya, Jide baada ya kutalakiana na mume wake ambaye pia alikuwa manaja wake, Gardiner G Habash, alimuomba Mosha kusimamia kazi zake za muziki na akakubali. Baadaye akakutana na Baraka The Prince katika uzinduzi wa wimbi wa Alikiba, akamuuliza kama angekubali kusimamia kazi zake na Baraka hakusita kukubali.

Gazeti la Daily Nation, linamuita malkia wa marejeo au kwa lugha ya kizungu ( Queen of comebacks). Hii ni kwasababu ya uwezo wake aliouonyesha, kuwarudisha kwenye game Alikiba akiwa na hit Mwana na Jaydee ambaye alirudi kwenye muziki kipindi ambacho nyimbo zake zilikuwa hazipati air play kwenye kituo cha redio cha Clouds FM ambacho ni muhimu sana kwenye ku-support wanamuziki wengi nchini Tanzania kwasababu za tofauti za kibinafsi ambayo baadaye ilitatuliwa.

Anasema hutumia pesa zake kwa kusafiri nchi tofauti tofauti za dunia, na kila mwaka huenda nchi tatu tofauti ambazo huwa ni geni kwake. Anapenda kupika na anapenda chakula kizuri pia.

Makala ya: Changez Ndzai (Kenya)
Facebook: Changez Ndzai
Twitter : @ChangezN
Instagram: changez_ndzai

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents