Michezo

David Beckham akanusha tuhuma kuwa alitumia uhusiano wake na UNICEF kusaka cheo cha ‘Usir’ Uingereza

David Beckham amekanusha ripoti kuwa alitumia uhusiano wake na shirika la umoja wa mataifa, UNICEF kupigia kampeni cheo cha ‘Usir’ nchini Uingereza.

Ijumaa, gazeti la Uingereza, The Sun, lilichapisha barua pepe zilizovuja, kati ya staa huyo wa soka na msemaji wake mwaka 2013 ambapo walijadiliana kuhusu kutafuta cheo (knighthood).

Kwenye barua pepe hizo, Beckham, aliyetunukiwa Order of the British Empire mwaka 2003, aliiita tuzo hiyo aliyopewa muimbaji Katherine Jenkins kuwa ni utani “a f**king joke,” na kuielezea kamati inayoamua nani anastahili kupewa heshima hiyo “bunch of c**ts.”

Msemaji wake amedaiwa kumsihi Beckham kujikita kwenye shughuli za kujitolea kama ubalozi wa UNICEF, ambao amekuwa nao tangu mwaka 2005. Jumamosi, msemaji wake, alimtetea baba huyo wa watoto wanne kuwa ripoti hizi zimemtengenezea picha ya tofauti kwa makusudi.

“David Beckham and UNICEF have had a powerful partnership in support of children for over 15 years. The David Beckham 7 Fund specifically has raised millions of pounds and helped millions of vulnerable children around the world,” yalisema maelezo yake.

“David Beckham has given significant time and energy and has made personal financial donations to the 7 Fund and this commitment will continue long term.”

Nayo UNICEF, ilitoa maelezo yake na kupongeza kazi za Beckham na shirika hilo.

“David Beckham has been a UNICEF Goodwill Ambassador since 2005, and as well as generously giving his time, energy and support to help raise awareness and funds for UNICEF’s work for children, David has given significant funds personally,” yamesomeka maelezo kwenye tovuti ya UNICEF.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents