Habari

Mfalme wa Thailand amuoa mlinzi wake na kutawazwa kuwa Malkia

Taarifa kutoka ndani ya ufalme wa Thailand zimesema kuwa, Mfalme Maha Vajiralongkorn ameamuoa kumuoa Naibu Mkuu wa kikosi cha walinzi wake na kupewa cheo cha malkia.

Picha iliyotolewa na ofisi ya Ufalme wa Thailand inaonyesha Mfalme wa Thai Maha Vajiralongkorn Bodindradebayavarangkun ( Kulia )akimmwagia maji Generali Suthida Vajiralongkorn na Ayudhya

Habari hizo za kushitukiza zimetolewa huku sherehe za kutawazwa kwake zikitarajiwa kuanza siku ya Jumamosi wakati atakapochukua wadhfa wake.

Taarifa kutoka kwenye ufalme huo zimesema ”Mfalme Vajiralongkorn ameamua kumpandisha cheo Generali Suthida Vajiralongkorn Na Ayudhya kuwa Malkia, atakuwa na cheo cha kifalme na hadhi kama sehemu ya familia ya kifalme”.

Mfalme Maha Vajiralongkorn mwenye umri wa miaka 66, alikuwa mfalme kikatiba baada ya kifo cha baba yake aliyependwa sana kilichotokea mwaka 2016.

Maha Vajiralongkorn amewahi wataliki wanawake mara tatu huku akiwa na ana watoto saba.

King Maha Vajiralongkorn na mpenzi wake , Generali Suthida Vajiralongkorn ambaye ametajwa kuwa Malkia Suthida katika harusi yao mjini Bangkok, Thailand Mei 1, 2019, k

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Malkia Suthida ni mpenzi wa muda mrefu wa mfalme Vajiralongkorn na amekuwa akionekana hadharani pamoja nae kwa miaka mingi, ingawa mahusiano yao kuwahi kuwa rasmi.

Picha kutoka katika sherehe za harusi zilionyeshwa moja kwa moja kwenye vituo vya televisheni vya Thailand Jumatano, ambapo watu wengine wa familia ya ufalme na washauri wa ufalme walihudhuria.

Mfalme alionekana akimwagia maji ya baraka Malkia Suthida kichwani. Baadae wawilI hao walisaini cheti cha ndoa.

Mnamo mwaka 2014 Vajiralongkorn alimteua Suthida Tidjai, ambaye ni mhudumu wa zamani wa Thai Airways, kama naibu kamanda wa kikosi cha walinzi wake. Alimpandisha cheo na kuwa Generali kamili jeshini Disemba 2016.

Mfalme aliyetangulia Bhumibol Adulyadej, alitawala kwa miaka 70 na kuwa ndiye mfalme aliyetawala kwa muda mrefu zaidi duniani na alifariki dunia mwaka 2016

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents