Mgomo Wa Walimu Ni Vituko Tu

WAKATI Katibu Mkuu Kiongozi na Mkuu wa Utumishi wa Umma, Phillemon Luhanjo, akipongeza kile alichokiita maelfu ya walimu kutounga mkono mgomo, wanafunzi wa shule za msingi katika maeneo mbalimbali jana waliandamana hadi ofisi za wakuu wa wilaya kueleza kilio cha kuwa hawafundishwi wala kufanya mitihani ya kumaliza mwaka.

 

WAKATI Katibu Mkuu Kiongozi na Mkuu wa Utumishi wa Umma, Phillemon Luhanjo, akipongeza kile alichokiita maelfu ya walimu kutounga mkono mgomo, wanafunzi wa shule za msingi katika maeneo mbalimbali jana waliandamana hadi ofisi za wakuu wa wilaya kueleza kilio cha kuwa hawafundishwi wala kufanya mitihani ya kumaliza mwaka.
Mbali na maandamano hayo, kukamatwa kwa viongozi wa Chama cha Walimu (CWT), mkoani Dodoma, shule nyingi kutoendelea na vipindi vya masomo, madai ya walimu kupunjwa malipo, baadhi kutoona majina yao, na matamko makali ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta), dhidi ya serikali vilitawala siku nzima ya jana kuashiria hali inazidi kuwa mbaya katika sekta ya elimu.
Katika taarifa yake ya jana kwa vyombo vya habari, Luhanjo, ambaye tangu Jumamosi amesimama kidete kuhakikisha walimu hawafanikiwi kugoma, alipongeza kile alichokielezea “maelfu ya walimu nchi nzima ambao wamekataa kushiriki katika mgomo usiokuwa na kikomo ulioitishwa na Chama cha Walimu (CWT)”, akisema kuwa huo ni “uamuzi wa busara na uzalendo unaojali masilahi mapana ya taifa letu.”
Lakini pongezi zake hazikulingana na hali halisi iliyotanda kwenye shule nyingi, hasa za msingi ambazo wanafunzi wake wengi walilazimika kuandamana hadi ofisi za halmashauri wakilalamika kuwa hawafundishwi wala kufanya mitihani yao ya kumaliza mwaka iliyokuwa ianze juzi.
Tukio kubwa kabisa likiwa la wanafunzi waliojitoa mhanga kutembea kwa mguu kutoka Mbagala, Kiburugwa hadi ofisi za mkuu wa wilaya zilizo pembeni ya Uwanja wa Taifa, ikiwa ni umbali wa zaidi ya kilomita 7, huku wakiimba, “tunataka haki zetu, tunataka haki zetu.”
Wanafunzi hao walioonekana kuchoshwa na urefu wa safari yao waliyoianza saa 2:30 asubuhi na kuimaliza saa 6:15, pamoja na jua kali lililotanda jana, waliungana na wengine kutoka shule za Kingungi, Serengeti, Ndalali na Muungano ya Chang’ombe kwenda ofisi za mkuu wa wilaya kulalamikia kitendo cha walimu kutoingia madarasani.

“Tulikuwa tunamtaka huyo afisa elimu ili tumueleze shida zetu, lakini tumeambiwa hayupo ofisini kwake na hatujui ameenda wapi,” alisema mmoja wa wanafunzi hao. “Sisi hatufundishwi, lakini wenzetu wameshafanya mitihani sisi hatujui tutafanya lini. Hapa tunamtaka mkuu wa wilaya tumueleze kwani tunaamini atatusikiliza na atatufikishia ujumbe huu panapohusika.

“Sisi hatufundishwi, walimu wanakuja shuleni wanatuangalia baadaye wanaondoka zao. Haya ni maandalizi gani, tutafeli!”

Wanafunzi hao walidai mbele ya afisa elimu wa Temeke, Hassan Kallinga kuwa wanadai haki yao kwa kuwa wamechanga fedha kwa ajili ya kufanya mtihani na hamna dalili zozote za kwamba watafanya mtihani.

“Tangu wiki iliyopita, shule ilipanga ratiba ya kwamba wiki hii, tungepaswa kufanya mitihani, na fedha tumeshachanga lakini cha kushangaza walimu hata darasani hawaingii, na mitihani hatufanyi, hivyo tumeamua kuandamana ili tujue haki yetu iko wapi na ni lini tutafanya hiyo mitihani,” alidai mwanafunzi mwingine.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents