Mgomo wa wanafunzi kuendelea juma tano

Baadhi ya wanafunzi jijini Dar es salaam walioandamana kupinga agizo la serikali kuongeza bei ya nauli za mabasi wamesisitiza kuwa wataendelea kuandamana hadi pale Serikali itakaposikiliza kilio chao.

Baadhi ya wanafunzi jijini Dar es salaam walioandamana kupinga agizo la serikali kuongeza bei ya nauli za mabasi wamesisitiza kuwa wataendelea kuandamana hadi pale Serikali itakaposikiliza kilio chao.

Akizungumza na waandishi wa habari Katibu Mkuu wa Chama cha Wanafunzi wa Sekondari Tanzania (TASSA Bw. Agustino Matefu alisema kuwa wameiandikia barua Serikali kuhusu kupunguziwa nauli na kuipa siku mbili kutoa majibu ambapo wasipojibiwa wataandamana nchi mzima bsiku ya jumatano.

Wakizungumza jijini Dar es Salaam, wanafunzi wengine walisema kuandamana kwao juzi kupinga nauli mpya ya sh. 100 si mwisho bali ni mwanzo wa kuendelea kudai haki yao ya msingi.

Walisema inasikitisha kuona wanafunzi wakipandishiwa nauli wakati Serikali inajua wazi wao hawafanyi kazi yoyote. "Sisi tutaendelea kundamana hata kama watakuwa wakitumwagia maji ya kuwasha na kutupiga mabomu ya machozi, ipo siku haki yetu itapatikana,"alisema mwanafunzi aliyejitambilisha kwa jina moja la Idd.

Alisema kusitishwa kwa maandamano hayo juzi haina maana wameshindwa kuyaendeleza, bali wanasubiri majibu kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Abbas Kandoro ambaye walifika ofisini kwake lakini hawakufanikiwa kumkuta.

Alisema wapo baadhi ya wanafunzi wamemua kuacha maandamano baada ya kupigwa na baadhi ya askari waliokuwa wakiwazuia lakini hiyo haiwazui wao kuendelea kuandamana na kudai haki yao.

Hata hivyo wakati wanafunzi hao wakipanga mikakati ya kundamana tena Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) jana walikutana kwa kikao cha dharura ambacho waandishi wa habari hawakuruhusiwa kuingia kusikiliza kinachojadiliwa.

Wakati huo huo baadhi ya wazazi wameunga mkono maandamano hayo yaliyofanywa na wanafunzi na kuitaka Serikali kuangalia upya suala la kupandisha nauli ya wanafunzi.

Bibi Rehema Juma mkazi wa Tandika jijini alisema hakukuwa na sababu kwa SUMATRA kupandisha nauli ya wanafunzi kwa kuwa kufanya hivyo ni kuendelea kuwatwisha mzigo wazazi.

Aliongeza kuwa yeye alitegemea nauli itabaki kuwa sh. 50 kwakuwa kuna kundi kubwa la askari ambao walikuwa hawalipi nauli na sasa wameamriwa kulipa na kufidia pengo la nauli ya wanafunzi.

Mkazi mwingine wa Airport Bi. Grace Gurisha, alitofautiana na wenzake na kusema maandamano hayo hayakupata kibali ndio maana kuna baadhi ya wanafunzi katika shule nyingine hawakufika kabisa.

"Mimi kama mzazi nina haki ya kulalamikia suala la nauli kupanda kwa wanafunzi… lakini watoto wetu utaratibu walioutumia sio sahihi na inaonyesha jinsi gani wasivyo na adabu" alisema Bi. Gurisha.

Kwa upande wa Bw. Matiko Musubi ambaye ni mfanyabiashara wa Ubungo-Terminal alieleza kwamba wanafunzi hao walikuwa wakifikisha kilio chao kwa viongozi wa Serikali na kusema kuwa walikuwa na hoja za msingi. Habari hii imeandikwa na Said Mwishehe, Prosper Mosha, Flora Amon na Frida Ally.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents