Habari

Mike Tee awachana NIDA

Mnyalu Mike T ameungana na watanzania wengine wengi wanaoulalamikia utaratibu unaotumiwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) katika kuandikisha wananchi.

Awali mamlaka hiyo ilitangaza kuwa zoezi hilo litahusisha mawakala watakaokuwa wakipita nyumba kwa nyumba kuandikisha wananchi wa Dar es Salaam ambako zoezi hilo limeanzia lakini utaratibu huo unadaiwa kutofanywa na hivyo wananchi kujiandika kwenye vituo.

Kupitia Facebook jana Mike T ameandika:

“Mimi nahisi hili suala la uandikishwaji wa vitambulisho vya uraia, kuna fungu lilitoka NAHISI la kuwawezesha mawakala kuzunguka majumbani kukusanya taarifa kama walivyoahidi mwanzo na nahisi tena kwa 70% haijafanyika hivyo ila kwenye ripoti zao za mapato na matumizi wataonyesha walifanya hivyo,Je majumbani kwenu wamepita? Kwetu hatujawaona kabisaaa.”

Katika zoezi hilo jijini Dar es Salaam wananchi wamelalamikua misururu mirefu ya watu katika maeneo mengi ya vituo vya uandikishaji.

Malalamiko mengine ni kuhusiana na maofisa wanaoandikisha watu kukosa uwezo wa kufanya kazi hiyo ya kuandikisha wananchi na Watendaji wa Serikali na wajumbe chama tawala kugeuza shughuli hiyo mradi wao.

Malalamiko mengine yaliyoibuka ni kuhusu muda uliowekwa ambao wengi wanasema ni mdogo na bado idadi kubwa ya wananchi haijafikiwa, licha ya kuongeza wiki moja baada ya Julai 30 iliyokuwa imepangwa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents