Misri Yaitolea Nje Stars

Timu ya soka ya taifa, Taifa Stars inatarajia kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa na timu ya taifa ya Msumbiji Novemba 19 kwenye Uwanja Mkuu wa Taifa, jijini, Dar es Salaam badala ya timu ya Misri, Pharaohs.

Timu ya soka ya taifa, Taifa Stars inatarajia kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa na timu ya taifa ya Msumbiji Novemba 19 kwenye Uwanja Mkuu wa Taifa, jijini, Dar es Salaam badala ya timu ya Misri, Pharaohs.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Afisa Habari wa Shirikisho la soka.

Tanzania (TFF), Florian Kaijage mechi dhidi ya Misri imeahirishwa kutokana na Chama cha soka cha Misri (EFA) kusema kuwa hawako tayari kucheza na Stars Novemba 19 na badala yake mechi hiyo ifanyike mwezi Januari mwakani.

Kaijage alisema kuwa TFF ilipokea barua kutoka EFA Novemba 2 na barua hiyo haikuweza kueleza sababu yoyote iliyowafanya waahirishe mchezo huo wa kirafiki kama walivyokubaliana.

Alisema kuwa TFF katika kuhakikisha kuwa Stars inapata mechi ya kujipima nguvu kabla ya kukutana na Sudan, ilianza mazungumzo na Chama cha soka cha Msumbiji (FMF) na kuweza kufikia makubaliano ya timu hizo kukutana.

“Jitihada zetu za makusudi zimeweza kuzaa matunda na hivyo TFF inapenda kuwajulisha kuwa Stars itacheza na Msumbiji Novemba 19 hapa jijini Dar es Salaam,“ ilisema taarifa hiyo.

Aliongeza kuwa FMF imeshaandika barua ya kuthibitisha kuleta kikosi imara kitakachoipa mazoezi mazuri Stars kama ilivyotarajiwa.

Alisema kuwa tayari FMF imeanza kuwasiliana na wachezaji wake wanaocheza soka la kulipwa katika nchi za Ulaya ili waweze kuja nchini kwa ajili ya mchezo huo unaotambulika na Shirikisho la soka la kimataifa (FIFA).

Awali TFF ilitangaza kuwa Misri ilikubali maombi yake na kuwataka wajiendae kwenda kucheza katika jiji la Cairo kufuatia timu yake ya taifa kuundwa na idadi kubwa ya wachezaji wa klabu ya Al Ahly ambayo inakabiliwa na mchezo wake wa fainali wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika wa marudiano uliopangwa kufanyika Novemba 16.

TFF iliialika Msumbiji mapema mwaka huu kuja kucheza na Stars lakini mchezo huo ulishindwa kufanyika kutokana na mvua kubwa kunyesha hapa jijini Dar es Salaam na uwanja wa Taifa uliotarajiwa kutumiwa ulijaa maji na hivyo FMF kuieleza TFF kuwa itakuwa tayari kucheza nayo siku nyingine.

TFF iliongeza kuwa tayari imeshampa taarifa Kocha Mkuu wa Stars, Marcio Maximo ambaye yuko kwao Brazil kwa mapumziko juu ya mabadiliko.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents