Miss Dar Indian Ocean 2010

Kampuni ya Frontline Management limited,ambayo kati ya wakurugenzi wake ni Mrembo wa Tanzania na Afrika 2005, Nancy Sumari, ndio waandaji rasmi wa mashindano ya miss Dar Indian Ocean 2010.Mashindano ya Miss Dar Indian Ocean yamekuwa na historia ya kutoa warembo wenye vigezo vya kimataifa tangu kuanzishwa.

Mashindano haya yametoa warembo wengi waliowania na kushinda taji la taifa na pia kusifika kama kitongoji pekee kilichotoa mrembo aliyefanya vizuri zaidi katika mashindano ya dunia na kushika taji la Miss World Africa. Historia ambayo haijapata mpinzani.

Nancy Sumari ni mrembo aliyetokea kitongoji cha Dar Indian Ocean na ndiye mrembo pekee ambaye ameweka historia mpaka sasa kwenye mashindano ya ulimwengu.

Warembo wengine ambao wametokea kitongoji hiki ni Richa Adhia ambaye kwa sasa ni Miss Tanzania India pamoja na Wema Sepetu anayeshughulika na sanaa ya uigizaji Tanzania.

Miaka michache iliyopita mashindno ya urembo yamepata sifa mbaya kwenye vyombo vya habari na kwa jamii kwa ujumla.
Nancy Sumari pamoja na timu yake ya Frontline Management, imeamua kuandaa mashindano haya sio tu kwasababu amewahi kuwa mshindi ndani ya kitongoji hicho, bali kwa dhumuni la kuleta mapinduzi katika mashindano ya urembo.

‘Dhumuni kubwa ni kuleta taswira  mpya katika mashindano ya urembo, kurudisha viwango vinavyotakiwa kwa warembo, kutambua mchango wao katika jamii na maendeleo kwa ujumla’, alisema Nancy.

Warembo wataandaliwa kisaikologia na kimashindano ili kuwa tayari kufanya vizuri katika mashindano ya Kanda na baadaye Taifa.
Warembo watashirikishwa pia kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo ya jamii na kuwa mabalozi wa kuleta utofauti kwenye jamii zinazowazunguka.

Haya yote yataleta taswira chanya kwa wadhamini na mashindano ya urembo kwa ujumla.
Frontline Management itatafuta na kuwafundisha wasichana wenye sifa na mvuto kushiriki katika mashindano ya Miss Dar Indian Ocean 2010.

Kutokana na uzoefu mkubwa waliokuwa nao kupitia ushiriki kwenye mashindano ya urembo na uaratibu wa matukio mbalimbali, tuna Imani ya kumtoa mrembo atakayetwaa taji la taifa pamoja na dunia, na kurejesha hadhi ya sanaa ya urembo nchini.

Warembo wanatarajiwa kufundishwa na Nancy mwenyewe pamoja na wakufunzi wengineo, lakini kwa upande wa suala zima la saikolojia, atakayewajenga katika hilo ni Sadaka Gandhi.

Tunapenda kuwakaribisha warembo wenye sifa waje kuchukua fomu za kushiriki shindano letu hilo tunalotegemea litakuwa la kihistoria kwa kutoa mrembo atakayekuwa Miss Kanda ya Kinondoni, Miss Tanzania na Miss World pia.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents