Miss Tanga patakuwa hapatoshi

Joto la Mchuano utakaofanyika keshokutwa jumamosi (Juni 7) wa kumsaka Mrembo wa Mkoani hapa Miss Tanga 2008, linazidi kupamba moto baada ya kila mshiriki wa shindano hilo kutamba kuwa ndiye atakayekuwa mrithi wa Victoria Martin.

JOTO la Mchuano utakaofanyika keshokutwa jumamosi (Juni 7) wa kumsaka Mrembo wa Mkoani Tanga Miss Tanga 2008 linazidi kupamba moto baada ya kila mshiriki wa shindano hilo kutamba kuwa ndiye atakayekuwa mrithi wa Victoria Martin.  

Wakizungumza na Bongo5 jana wakiwa kwenye kambi yao iliyopo Splended huko Tanga warembo hao walisema wamenolewa kiasi kikubwa na pataleta ushindani mkali katika kinyang’anyiro hicho.  

Warembo watakaochuana kusaka taji hilo ni Mariam Mhando,Doris Steven,Judith Assey,Amina Sadick,Halima Khalfan,Aisha Abdallah,Nuru Salim,Beatrice Lwimba,Oliver Mangona Mwajuma Msangi.  

Wengine ni Agnes Mwakipesile,Hadita Ramadhani,,Hawa Njama,Mariam Ajibu,Marie Fredrick, na Evelyine Thomas.  

Mkurugenzi wa Kampuni ya  Five Brothers Promotions inayoandaa mashindano hayo, Nassor Makau alisema jana kuwa maandalizi ya shindano hilo yamekamilika na kwamba limepangwa kufanyika Uwanjwa wa Mkwakwani Tanga.  

Aidha aliongeza kusema shindano hilo litapambwa na burudani ya muziki wa dansi kutoka Bendi ya Akudo Impact yenye makao yake Jijini Dar es salaam inayotumia mtindo maarufu wa Pekechapekecha.  

Alayataja makampuni yaliyojitokeza kudhamini shindano hilo ni pamoja na Mwananchi Communication,Vodacom, reds, Tanga Fresh, Sofia Production, Hotel ya Kola Prieto na Benki ya CRDB.  

Mpaka sasa Taji la Miss Tanga,linashikiliwa na Victoria Martin ambaye pia alinyakuwa ushindi wa Miss Kanda ya Kaskazini na hatimaye kuwa Balozi wa Reds.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents