Miss Tanzania 2008…Ni Nasreem Karim

Shindano la kumtafuta mlimbwende wa Tanzania hatimae jana liliweza kufikia kileleni baada ya jopo la majaji kumteua mwanadada Nasreem Karim (22) kuwa ndiye mshindi aliyeweza kujinyakulia taji hilo kwa mwaka 2008….

miss_tz_2008_6.jpg

 

Shindano la kumtafuta mlimbwende wa Tanzania hatimae jana liliweza kufikia kileleni baada ya jopo la majaji kumteua mwanadada Nasreem Karim (22) kuwa ndiye mshindi aliyeweza kujinyakulia taji hilo kwa mwaka 2008, huku akiiwakilisha kanda ya ziwa ambayo mwaka huu imetoka kifua mbele kabisa.

Shindano hilo la Vodacom Miss Tanzania lilidhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom na kuweza kufanikisha azma yao ya kumfukunyua mrembo wa mwaka 2008.

Jumla ya warembo 27 kutoka sehemu na vitongoji mbali mbali waliweza kupita jukwaani kuigombea nafasi hiyo, halikadhalika majaji walionekana kuwa na wakati mgumu sana kwani kila mrembo aliyekatiza jukwaani alikuwa ni mzuri na mwenye kuvutia.

Kama ilivyo kawaida ya Shindano la Vodacom Miss Tanzania humteua baozi wa redds ambaye mwaka jana nafasi hiyo ilichukuliwa na mlimbwende Victoria Martin lakini mwaka huu nafasi hiyo imenyakuliwa na mwanadada Angela Lubala ambaye anaiwakilisha Temeke.

Wakati huo huo kwa mara ya kwanza tume inayojihusisha na masua ya ukimwi ya Tacaids nayo haikuwa nyuma kwani ilichagua balozi wao ambaye ataiwakilisha katika mapambano ya kuzuia kuenea kwa janga hatari la ukimwi ambapo warembo wote waliweza kujipatia mafunzo kuhusiana na masuala ya ukimwi walipokuwa kambini na Sylivia Mashuda aliweza kujinyakulia taji hilo pamoja kitita cha shilingi milioni moja.

Baada ya kazi kubwa iliyofanywa na majaji hatiamaye mchujo ulifanyika na tano bora kupatikana ambapo walijibu maswali na mwisho kabisa Miss Tanzania mstaafu Richa Adhia aliweza kutoa risala fupi kabla kukadhi taji kwa mshindi ambaye kwa wakati huo hakuwa akifahamika.

Mara Mwanadada Pendo Lizer (22) ambaye alikuwa ni Miss Higher Learning litangazwa kuwa ni mshindi wa tatu, akifuatiwa na Sylivia Mashuda (19) ambaye alichukua nafasi ya pili, na hapo kila mtu alikaa mkao wa kusikiliza nani atasimikwa taji la Miss Tanzania 2008…..Na Miss Tanzania 2008 ni Nasreem Karim……watu weweweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.

Aidha Miss Tanzania 2008 aliweza kujinyakulia zawadi ya gari aina ya grand vitara na fedha taslim.

 miss_tz_2008_7.jpg

Miss Tanzania 2008 Nasreem Karim akijibu swali toka kwa Jaji Shose Sinare.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents