HabariPicha

Miss Universe Tanzania aenda Mexico

Miss Universe Tanzania 2007Miss Universe Tanzania, Flaviana Matata ameondoka jijini jana kwenda Mexico, tayari kwa mazoezi ya mwezi mmoja kwa ajili ya mashindano ya Miss Universe ya dunia


Na Majuto Omary

Miss Universe Tanzania, Flaviana Matata ameondoka jijini jana kwenda Mexico, tayari kwa mazoezi ya mwezi mmoja kwa ajili ya mashindano ya Miss Universe ya dunia yaliyopangwa kufanyika Mexico City Mei 28.

Flaviana aliondoka kwa ndege ya Oman Air na ameahidi kufanya makubwa katika mashindano hayo ambayo Tanzania inashiriki kwa mara ya kwanza.

Alisema kuwa atajitahidi kuweka historia kwa Tanzania ili kuitangaza kwa nyanja zote, za kisiasa, utalii, uchumi na amani Duniani.

“Nimefanya maandalizi chini ya mratibu wa Taifa wa mashindano hayo, Maria Sarungi na Magreth Wilson Chacha ambaye ana uzoefu wa kimataifa katika mashindano ya dunia,” alisema Flaviana.

Aliwataka Watanzania kumsapoti kwa njia moja au nyingine ili kuweza kuibuka kidedea katika mashindano hayo makubwa kushinda yale ya Miss World.

Alisema kuwa sara za Watanzania na maandalizi yake ndiyo nyenzo tosha ya kuwachanganya washiriki wengine na hata majaji ili kuibuka kidedea.

Mbali ya kuwania taji la Miss Universe la Dunia, mrembo huyo pia atawania mataji mengine kama mrembo bora anayeonekana katika picha, Miss Photogenic na Taji la mrembo mchangamfu au mcheshi `Miss Congeniality’.

Mratibu wa mashindano hayo kwa hapa nchini, Sarungi ataondoka jijini siku chache kabla ya mashindano hayo kufanyika.

Source: Mwananchi

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents