Burudani ya Michezo Live

Mke wa rais wa Burundi Denise Nkurunziza, atoa wimbo ukizungumzia unyanyasaji wa wanawake – Video

Mke wa rais wa Burundi Denise Nkurunziza, atoa wimbo ukizungumzia unyanyasaji wa wanawake - Video

Mke wa rais wa Burundi Denise Nkurunziza ametoa wimbo wa kampeni ya kupambana unyanyasaji wanawake wanaoshindwa kupata ujauzito hukabiliana nayo.

Ukanda wa video wa wimbo huo unaanza kwa picha ya mwanamke anayemkaribisha mume wake nyumbani na kumkaribisha kula chakula cha jioni ambaye anamtemea mate ghafla na kumpiga.

“Hauna maanakatika nyumba hii ,” asema. “Tumbo lako kila wakati limejaa maharage, huku matumbo ya wanawake wengine yamejaa watoto wachanga.”

Bi Nkurunziza, mwenye umri wa miaka 49, anaonekana akiingilia kati, akiingia katika sebule ya wanandoa wasio na wa mtoto. Alisikika mwenye akitoa ushauri wa maridhiano, akielezea kwamba: “kusema ukweli unafahamu kuhusu kutokuwa na uwezo wa kuzaa tu baada ya kumuona daktari.

“Suala la kutokuwa na uwezo wa kuzaa linaweza kutokea kwa mwanaume au mwanamke .” Katika picha inayofuatia, Mke wa rais, anaonekana akiimba, akidensi na wanenguaji pamoja na wanamuziki wengine.

“Wanawake hawakuumbwa kuitwa mama tu. Wana uwezo wa kufanya mambo mengine mengi ,” kibwagizo kinaendelea cha wimbo huo

Nkurunziza na mkewe wakipanga mstari kwa ajili ya kupiga kura mwaka 2018, wameoana kwa miaka takriban 25Haki miliki ya pichaAFP
Image captionNkurunziza na mkewe wakipanga mstari kwa ajili ya kupiga kura mwaka 2018, wameoana kwa miaka takriban 25

Mke wa Nkurunziza, ambaye ameolewa na rais Pierre Nkurunziza tangu 1994, anawatolea wanaume waliooa kuwasaidia wake zao.

” Kutokuwa na uwezo wa kuzaa kunawahusisha watu wawili na kutokuwa na uwezo wa kuzaa hakupaswi kuwa chanzo cha mzozo,” anaimba.

Nkurunziza na mkewe ambao wana watoto watano pamoja na kuwaasili wengine kadhaa , wanafahamika kuwa ni watu walioshika dini sana na mara kwa mara wamekuwa wakiandaa mikutano ya maombi pamoja.

Bi Nkurunziza, ambaye wakati mmoja alifanya kazi kama afisa wa uhamiaji, ni mchungaji aliyetawazwa.

Wimba wake huo mpya kwa jina – Umukenyezi Arengeye Kuvyara Gusa (mwanamke ni zaidi ya kuzaa tu ) – ambao ulishirikishwa katika mtandao wa WhatsApp mapema wiki hii inaonekana kuwa ni mara ya kwanza kutoa video ya wimbo usio wa kidini.

Bi Nkurunziza amekuwa akionekana wakati mwingine katika nyimbo za kidini, na katika kwaya ya kanisa.

Video hiyo ya dakika nne pia imeshirikishwa katika mtandao wa Facebook:

Denise Nkurunziza akiimba katika wimbo wake mpyaHaki miliki ya pichaPAPY JAMAICA
Image captionDenise Nkurunziza akiimba katika wimbo wake mpya

Mke huyo wa rais amepata sifa kutoka kwakatika mitandao ya kijamii kutokana na video yake ya hivi karibuni, ingawa baadhi wamesema wanaume wanaweza pia kukabiliwa na unyanyasaji kutoka kwa wake zao.

Katika jamii ya Burundi yenye mfumo dume, wanandoa wanafanywa wajihisi kuaibika pale wanapokuwa hawana watoto – na kutokuwa kwao na kwa kawaida mwanamke huwa ndiye anayelaumiwa pale wanandoa wanaposhindwa kupata mtoto. Baadhi ya wanandoa hulazimika kuachana kutokana wanaposhindwa kuzaa pamoja.

Chanzo BBC.

By Ally Juma

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW