Burudani

Mkongwe Stevie Wonder alivyoipigia magoti Marekani kwenye GCF (Video)

Mkongwe wa muziki duniani Stevie Wonder inawezekana ameona mbali katika utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump, ambapo rais huyo ameonekana kutengeneza maadui wengi zaidi hasa vita ya maneno iliyopo kati yake na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un.

Jumamosi hii msanii huyo aliamua kupiga magoti mbele ya mashabiki kwa kuiombea Marekani na dunia nzima kwa ujumla katika tamasha la Global Citizens Festival lililofanyika mjini New York.

“Usiku huu, ninapiga magoti kwa Marekani; lakini sio goti moja, napiga magoti yote. Magoti yote ni maombi ya dunia yetu, kwa baadae, viongozi wetu wa dunia na dunia yetu. Amiina,” alisema Stevie Wonder kabla ya kutumbuiza katika tamasha hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents