Burudani

Mlango wa BBA 6 wafunguliwa

barbara_dstv

KAMPUNI ya MultChoice Afrika, imezindua awamu ya sita ya shindano la Big Brother Africa ambapo milango ya washiriki kuanza kuomba ushiriki imefunguliwa.

Akizungumza Dar es Salaam jana Meneja Uhusiano wa MultChoice Tanzania, Barbara Kambogi alisema kuwa anakaribisha Watanzania ambao wanataka kushiriki shindano hilo kuhakikisha wanatumia nafasi hiyo ipasavyo na kuwasilisha maombi yao kwa muda unaopasa.

Alisema katika shindano la mwaka huu ambalo mshindi ataondoka na dola za Marekani 200, 000 litashirikisha washiriki 14 katika nchi 14 za Afrika, zikiwemo Angola, Botswana, Ethiopia, Ghana, Kenya, Malawi, Msumbiji, Namibia, Nigeria, Afrika Kusini, Tanzania, Uganda, Zambia na Zimbabwe.

Barbara alisema fomu za ushiriki zinapatikana ofisi za MultiChoice Tanzania, na pia kupitia mitandao ya www.mnetafrica.com/bigbrother au [email protected] na kuwa mwisho wa kurejesha fomu ni Februari 27 2011.

Alisema kuwa shindano hilo ambalo washiriki watakaa kwa siku 91, linatarajia kuanza Jumapili ya Mei Mosi, mwaka huu, na kurushwa moja kwa moja kwa watazamaji wote wenye king’amuzi cha DSTV.

Tangu kuanza kurushwa kwa shindano hilo mwaka 2003, tayari mashindano matano yamefanyika huku washindi kadhaa kujinyakulia zawadi.

Ushindi wa shindano la kwanza ulikwenda kwa Cherise Makubale wa Zambia aliyefuatiwa na Mwisho Mwampamba wa Tanzania. Shindano la pili alikuwa ni Mtanzania Richard Bezuidenhout na baadaye Muangola Ricco Venancio alikuwa mshindi wa shindano la tatu.

Mshindi wa shindano la nne alikuwa ni Kevin Pam Chuwang na yule wa shindano la tano akiwa Uti Nwachukwu, wote wakiwa wametokea Nigeria.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents