Habari

Mlanguzi mkuu wa madawa ya kulevya Mombasa na baadhi ya vigogo kuhukumiwa Marekani

Hukumu ya anayetajwa kuwa mlanguzi mkubwa wa dawa za kulevya Baktash Akasha inatarajiwa kutolewa baadae leo mjini New York nchini Marekani.

Akasha Brothers

Baktash na nduguyake Ibrahim walikamatwa mjini Mombasa mwaka 2014 wakiwa pamoja na raia kutoka Pakistani na mwingine wa India.

Ndugu hao wa Akasha wanatuhumiwa kutumia ghasia, mauaji na kutoa hongo kulinda biashara yao. Wanatuhumiwa kupanga mauaji ya mhalifu raia wa Afrika Kusini anayefahamika kwa jina moja pekee ‘Pinky’.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Hukumu hiyo inatarajiwa leo wakati taarifa zinaeleza kuwa afisa wa zamani katika idara ya upelelezi nchini DCI, majaji kadhaa na maafisa wengine wa serikali huenda wakahamishwa kupelekwa Marekani kukabiliwa na mashtaka yanayohusu ulanguzi wa madawa ya kulevya.

Gazeti la Nation nchini Kenya linaripoti kuwa duru zinaarifu kwamba serikali ya Marekani tayari imeifahamisha kuhusu nia hiyo ya kuwashtaki washukiwa katika mahakama za Marekani.

Hatua inayomaanisha kwamba huenda katika siku zijazo kukashuhudiwa kuwasilishwa kwa washukiwa kwa maafisa wa usalama Marekani.

Athari ya madawa ya kulevya kwa vijana Mombasa

Mji wa Mombasa katika pwani ya Kenya unapitia madhara mengi ya dawa za kulevya, huku familia hiyo ya Akasha ikilaumiwa kuchangia janga hilo pakubwa.

Mwandishi kutoka eneo hilo Francis Ontomwa anaeleza kwamba unapolitaja jina la Akasha mjini Mombasa, linaibua uoga na wasiwasi mwingi.

Kwa miaka kadhaa, familia ya Akasha iliendesha na kujenga himaya ya ulanguzi wa madawa ya kulevya, kutoka kitovu cha Mji huo wa Mombasa, kufikia Afghanistan, Ulaya na hata nchini Marekani.

Madhara ya biashara hiyo yanaonekana wazi katika mji huo wa pwani ya Kenya.

Salma Hemed ni mwanaharakati wa kutetea haki za ibnaadamu kutoka shirika la Haki Afrika ambalo limekuwa likijishughulisha na harakati za kupambana na madhara biashara hiyo haramu miongoni mwa vijana.

‘Kwa wale wenye kuuza wanahitaji vijana wa kutoka nyanjani tofuati. Na katika kuonja mihadarati, inawafanya wao waanze kuwa watumiaji wakuu na pia kutegema pakubwa (waraibu) na kuanza kuwa watumiaji mihadarati’.Takriban watu wanane wamejeruhiwa baada ya vijana waliojihami kwa mapanga kuushambulia mtaa wa Kisauni mjini Mombasa.

Takriban watu wanane wamejeruhiwa baada ya vijana waliojihami kwa mapanga kuushambulia mtaa wa Kisauni mjini Mombasa.

Uhalifu uliokithiri Kisauni

Kisauni ni sehemu mojawapo ya mitaa maskini Mombasa.

Ni eneo linalokabiliwa na uhaba mkubwa wa usalama. Wiki iliyopita watu wanane walijeruhiwa vibaya na gengi la majambazi.

Utumiaji mihadarati umekithiri pakubwa miongoni mwa vijana katika mktaa huo.

‘Sisi letu kubwa ilikuwa ni kuwakanya na kuiambia serikali kwamba wale ambao wanahusikana mambo kama haya wasiwahurumie’ anasema mkaazi mmoja.

Ni miongo miwili tangu babayao ndugu wawili wanaosubiri kuhukumiwa leo – kuuawa huko Amsterdam nchini Uholanzi.

Kuuawa kwa mzee Akasha kunahusishwa na biashara ya ulanguzi wa mihadarati.

Baadhi ya wakaazi wanadai kuwa familia ya Akasha imlifanikiwa kukita mizizi na kujenga himaya yao Mombasa, kutokana na rushwa na kuhongwa kwa maafisa wa idara za sheria na haki.

Baktash mwenye umri wa miaka 42 anatarajiwa kuhukumiwa leo na mahakaman ya wilaya ya kusini New York na nduguye Ibrahim anatarjiwa kuhukumiwa Novemba 8 baada ya wote kukiri mashtaka yaliowasilishwa dhidi yao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents