Habari

Moto wateketeza soko Morogoro

KILIO kikubwa kilitawala miongoni mwa wafanyabiashara wa soko la mitumba la Sabasaba baada ya moto ambao haujajulikana chanzo chake kuteketeza mali zote na maduka yanayozunguka soko hilo lililopo uwanja Sabasaba.

Na Ramadhan Libenanga , Morogoro

 

KILIO kikubwa kilitawala miongoni mwa wafanyabiashara wa soko la mitumba la Sabasaba baada ya moto ambao haujajulikana chanzo chake kuteketeza mali zote na maduka yanayozunguka soko hilo lililopo uwanja Sabasaba.

 

Mwandishi wa habari hizi alishuhudia tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana saa 2:30 huku wafanyabiashara hao wakihangaika kuokoa mali zao na wengine wakiangua vilio.

 

Moto huo ulianzia katika stoo ya kuhifadhia mizigo ya wafanyabishara hao zaidi ya 1,000 na kuteketeza mali zao zote katika stoo hiyo na kuenea hadi kwenye maduka yanayozunguka uwanja huo.

 

Pamoja na jitihada za vikosi vya magari ya zimamoto ya Manispaa, moto huo uliendelea kuwaka kwa kasi huku na kuendea kwenye maduka mengine.

 

Baadhi ya wafanyabiashara hao walisikika wakidai kuwa moto huo umewapa hasara kubwa kwani hawajui namna watakavyoresha mikopo waliyochukua kuanzisha biashara zao.

 

“Kwa kweli umasikini umetukumba tulikokopa tunatakiwa kuendelea kulipa madeni hatujui tutafanyaje,“ alisikika akisema mmoja wa wafanyabiashara hao aliyejitambulisha kwa jina la Bi. Manka Mushi.

 

Wafanyabiashara hao wamemuomba Rais Kikwete kukemea urasimu katika upatikanaji wa mikopo katika asasi za kifedha kwani walisema pamoja na nia nzuri ya Serikali kutoa pesa za mikopo wanashindwa kunufaika kutokana na urasimu uliopo.
kama ilivyo
Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Bw. Thobias Andengenye alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lakini alisema Jeshi la Polisi bado halijajua chanzo cha moto huo na uchunguzi unaendelea ikiwa ni pamoja na kujua thamani ya mali zilizoungua.

 

Source: Majira

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents