Burudani

Motra The Future atoa siri ya kufanya remix ya Waka kutoka kwa Diamond (+audio)

Msanii wa muziki Bongo, Motra The Future amefunguka sababu ya kufanya remix ya ngoma ya Diamond ‘Waka’ ambayo muimbaji huyo amemshirikisha Rick Ross.

Motra ameiambia Bongo5 sababu ya kufanya remix ya ngoma hiyo ni kumbumbusha Diamond kuhusu kauli yake aliyotoa kuwa moja marapa ambao anatamani kufanya nao ngoma ni Motra The Future.

“Nilifanya vile kama statement ya kumkumbusha kuhusiana na kauli yake ambayo aliitoa lakini kwa sababu najua ni brother mishe nyingi, yupo bize nikaona nitengeneze ili atatakaposikia akumbuke,” amesema Motra.

Pia amesema kuhusu kufanya video ya ngoma hiyo ni hadi pale atakapowasiliana na uongozi wa Diamond. Katika Hatua  nyingine Motra amezungumzia ngoma yake mpya ‘Mwajuma chaUtudu’.

Msikilize hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents