Michezo

Mourinho: Abramovich yupo pamoja na mimi

Kocha wa Mabingwa watetezi wa ligi ya England, Chelsea, Jose Mourinho amesema mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich yuko pamoja naye licha ya msimu mbovu wa mabingwa hao wa England.

2F2BB2CC00000578-3350987-image-a-18_1449580241332

Hadi sasa Chelsea wapo nafasi ya 14 kwenye ligi kuu England baada ya kupoteza mechi 8 za ligi kati ya 15. Leo Jumatano Desemba 9 wanacheza mechi ya mwisho ya kundi lao na FC Porto wakihitaji sare tu au ushindi ili kusongambele.

Akiongea kuhusu kuelekea mechi ya UCL, Mourinho, alipoulizwa kama atabakishwa kama meneja wa Chelsea, alijibu: Nadhani nimefanya mengi mazuri kwa klabu hii, sidhani mmiliki ni mtu anayeyumbayumba.”

Mourinho, leo Jumatano anapambana na klabu ya kwao Ureno, FC Porto ambayo aliwahi kuwa kocha wao, ameeleza: Abaramovich ameniamini mara mbili.

Huku kukiwa na uvumi kuwa Mourinho atatimuliwa ikiwa atafungwa mechi mbili mfululizo na mechi ya leo na FC Porto na kufuatia kipigo cha Bournemouth, kwenye mechi ya ligi Jumamosi iliyopita.

Jumatatu ijayo, Chelsea itacheza na vinara wa Ligi Leicester City.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents