Michezo

Mourinho aendeleza msimamo wake ” Manchester United bado ina msimu mgumu licha ya kushinda mfululizo”

Mourinho aendeleza msimamo wake " Manchester United bado ina msimu mgumu licha ya kushinda mfululizo"

Kocha wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho amesema licha ya timu yake kushinda michezo mitatu mfululizo hayawezi kubadili msimamo wake kuhusu timu hiyo kuwa Manchester United bado iko katika hali ngumu ina msimu mgumu.

Kocha huyo Ureno alitabiri mwanzoni kuwa timu hiyo ina wakati mgumu kuitetea nafasi yake katika ligi licha ya kushinda hiyo michezo mitatu ambayo ni naina ya Burnley, Watford na Young Boys, na kuongeza ushindi huo hauwezi kubadili mawazo yake.

Mourinho alisema “Nina matumaini, lakini tuna msimu mgumu,” alisema. “Kiukweli tuna msimu mgumu na tuna hali ngumu siwezi kubadili msimamo wangu eti kwa sababu tulishinda mechi mbili mfululizo katika Ligi Kuu.”

“Unaona kiwango cha timu nyingine kubwa katika ligi hii, umeona kikosi cha Liverpool, kikosi cha Man City, kikosi cha Chelsea, kikosi cha Tottenham, na hata kikosi cha Arsenal ingawa kinazidi kuboreka,kwa upande wetu bado ni vigumu.”

Mourinho alisema timu inatakiwa kukusanya  pointi 81 ambazo zilikusanywa msimu wa mwisho wa Sir Alex Ferguson kabla ya kustaafu mwaka 2013

United watakuwa na mchezo dhidi ya  Wolves siku ya Jumamosi na wana nafasi ya  kushinda michezo minne mfululizo kwa mara ya kwanza tangu Januari, na Mourinho amesema ana uhakika timu yake imeongeza ubora  kutoka msimu uliopita.

“Sisema tutaweza kuwa na pointi zaidi kuliko msimu uliopita,” alisema. “Nadhani tutakuwa timu bora zaidi. Tutaweza kucheza vizuri zaidi kuliko msimu uliopita”

“Sio tu kwa ajili yetu, pia kwa ajili ya wengine, wengine, wanaweza kusema sawa na mimi na wanaweza kusema ‘oh, Manchester United, timu nzuri,ina kikosi mzuri, kikosi kizuri zaidi ya City, watu wanaweza kusema hivyo.”

By Ally Juma

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents