Michezo

Mourinho atoa majibu kuhusu tuhuma zake za kutoa lugha chafu mbele ya Kamera

Kilikuwa kidole kama vidole vingine vya kawaida

Kocha wa Manchester United Mreno Jose Mourinho ameweza kujieleza kwa kile kilichosemekana ametoa lugha chafu mbele ya kamera katika mchezo uliowakutanisha dhidi ya Newcastle United katika dimba la Old Trafford.

Mourinho alionyesha kidole kidogo cha mwisho mbele ya kamera huku akionekana anatoa maneno fulani ambayo yalisemekana sio  maneno ya busara ambayo aliyaongea Mreno huyo.

Shirikisho la soka nchini Uingereza FA lilitoa kauli ambayo ilimtaka kocha huyo kutoa maeleza kuhusu video na picha  ambazo zilionekana zinatembea kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha anatoa maneno fulani ambayo yalikaririwa hayakuwa mazuri.

Kauli ya FA ilikuwa inasema;-  “Inasemekana kwamba lugha yake mwishoni baada ya matokeo hayo, kama ilivyotumwa na kuonekana katika video na picha mbalimbali, ilikuwa ya dharau, matusi na ikionekana isiyofaa kabisa, Hivyo Mourinho anatakiwa kujibu tuhuma hizi hadi ifikapo Octoba 19 muda wa saa kumi na mbili jioni”

Na baada ya kauli hiyo ya FA ambayo ilimtaka Mreno huyo kutoa maelezo kabla ya Octoba 19 ambayo ni siku ya Ijumaa,Mourinho siku ya Jumatano amefunguka kuhusiana na sakata lake hilo la kuonekana kwenye kamera akitoa maneno machafu, Kwa kadiri tunavyojua, hakuwa ameshtakiwa kwa kuonyesha kidole kidogo hewani wakati akizungumza kwenye kamera, ishara fulani ilitiliwa mkazo ambayo haikuwa nzuri.

Mourinho amesema:- ” kile kilikuwa ni kidole tu,kama vilivyokuwa vidole vingine vya kawaida” Mourinho aliongeza  “Sio kidole nilichokuwa nikicheza na Tito Vilanova kwenye jicho miaka mingi iliyopita na wala sio kidole ambacho mimi nakitumia kuvalia pete yangu ya keki ya ndoa, au sio kidole cha katikati ambacho Napenda kuwaonyesha watu wanaouliza maswali ya kijinga pia hakikuwa hicho.”

Huku kocha huyo akijitetea kuwa maneno hayo huenda yalikuwa ya Kireno na kuwauliza “wataalam wa lugha” Kama mnaweza kusoma midomo inavyoongea kwa lugha ya kireno usingekuwa na uhakika wa kile ulichosema”.

Katika picha zinazotembea zilionyesha nyama za midomo ya Mourinho zikitamka maneno haya:- “f— off, sons of a b—-.” (Or, more plausibly, “sons of b—-es,”

Manchester United Octoba 20 inasafiri hadi katika jiji la London kukutana na Chelsea ambao wameanza vizuri msimu huu wakiwa katika nafasi ya pili na alama za 20 huku United wakiwa katika nafasi ya 8 na alama zao 13.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents