Habari

Mpishi wa Kenya avunja rekodi ya dunia, apika vyakula 400 kwa muda huu, Gavana Joho amuandikia ujumbe mzito

Maliha Mohammed mpishi maarufu kutoka Mombasa nchini Kenya amevunja rekodi ya dunia ya kitabu cha Guiness kwa kupika kwa muda mrefu zaidi.

Maliha Mohamed

Mwanamke huyo amekuwa mtu wa kwanza kuvunja rekodi hiyo barani Afrika.

Maliha alipika kwa muda wa saa 75 bila kusita na hivyobasi kuvunja rekodi ya dunia siku ya Jumapili katika hoteli ya kitalii ya Bay Beach mjini Mombasa.

Muda mrefu zaidi kuwahi kufikiwa ulikuwa muda wa saa 68 dakika 30 na sekunde 1, na ulivunjwa na Rickey Lumpkin mjini Los Angeles Marekani mwaka 2018.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 36 alikuwa ameandaa mapishi 400 ya nchini na kimataifa kwa ajili ya mashindano hayo ili kuweka jina lake katika kitabu hicho cha rekodi za dunia cha Guiness.

Vyakula alivyoandaa vitatolewa kwa nyumba za hisani na zile za mayatima kama mojawapo ya kutoa hamasa na kuwasaidia wasiojiweza mjini Mombasa.

Gavana wa Mombasa, Ali Hassan Joho kupitia akaunti yake ya facebok ameandika ujumbe wa kumpongeza mwanadada huyo kwa hatua kubwa aliyofikia na si kwaajili ya Kenya pekee bali ni pamoja na bara zima la Afrika.

https://www.facebook.com/alihassanjoho/photos/a.535577493167268/2433475996710732/?type=3

Katika jaribio lake la kwanza mwezi Mei mwaka huu, mama huyo wa watoto wawili alipika vyakula 100 katika muda wa saa 36 bila kusita.

Baadaye mwezi Julai, mpishi huyo alipika vyakula 200 kwa saa 54 kabla ya kuelekea katika fainali iliosimamiwa na maafisa wa kitabu hicho cha rekodi za dunia za Guiness.

Akisaidiwa na takriban watu 40 waliokuwa wakifanya kazi kwa zamu , Bi Mohammed awali alikuwa ameonyesha matumaini ya kuweza kushinda rekodi.

Juhudi zake za kushindana 2018 anasema zilifeli kutokana na matatizo ya kifedha.

Kitabu cha rekodi za dunia za Guinness huchapishwa kila mwaka, kikiorodheshwa rekodi za dunia zilizovunjwa na binadamu.

“Niliwasilisha ombi langu mnamo mwezi Disemba kwa Guiness Book na wakajibu mwezi Aprili mwaka huu kwamba ombi langu la saa 75 lilikubaliwa” , Maliha alisema akizungumza na gazeti la The Star nchini Kenya.

https://www.facebook.com/FreshFriCookingOil/videos/394946327879823/?t=5

Alifadhiliwa na kampuni ya mafuta ya kupikia ya Pwani Oil Products Limited, ambao walimsaidia katika kumpatia mafuta hayo na vitu vingine vinavyohitajika katika mapishi huku wahisani wengine wakimsaidia na jiko la kupikia.

‘Mwaka uliopita nilipojiondoa katika mashindano sikuvunjika moyo. Kupitia fedha kidogo nilizokuwa nimechangisha , niliamua kubadilisha sebule yangu kuwa jiko na nikiwa na marafiki zangu 20 tulipika kwa zaidi ya saa 72 bila kusita”, alinukuliwa na gazeti la The Star daily akisema.

https://www.facebook.com/photo.php?fbid=2377750688967867&set=a.163094800433478&type=3

Maliha anasema kwamba alipata msukumo wa kuingia katika shindano hilo kama njia ya kuisaidia jamii.

https://www.facebook.com/maliha.islam.395/videos/2419378341463950/?t=0

Aliyekuwa akishikilia rekodi hiyo Rickey alijaribu kuvunja rekodi hiyo ili kuchangisha fedha kuwafadhili watoto kupitia shirika lisilo la serikali la World Vision.

”Nikiwa na miaka 36 nataka kuwa mfano wa kuigwa kwa wasichana wangu na jamii katika eneo ninalotoka”, anasema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents