Tupo Nawe

Mr Blue akanusha kuwa na bifu na Diamond

Mr Blue ameamua kuweka wazi kuhusu taarifa za muda mrefu zilizosambaa kuwa hana maelewano mazuri na Diamond Platnumz.

Hit maker huyo wa Mbwa Koko, ameiambia Wasafi TV kuwa watu ndio wanataka kuwaingiza kwenye matatizo, ila yeye ndio ameanza kumsupport Diamond tangu chini kabisa akiwa hajulikani na mtu yoyote hata waandishi wa habari.

“Ukikaa na Diamond ukimuuliza atakujibu kwamba mimi nimeanza kumsupport since day one, tokea Diamond hajulikani na waandishi wa habari, hajulikani na mtu yoyote. Alinifuata kama brother wake nikamsupport kwenye muziki wake,” amesema Mr Blue.

“Kwa mfano huo rahisi unaonyesha mimi sina chuki na Diamond, wala sina tofauti yoyote. Kama ningekuwa na tofauti ningemzuia tokea awali hata nyinyi msingepata ajira, kama ningemzuia kule mwanzoni nisinge msupport. Amekuja amekuwa msanii mkubwa ametengeneza kama hii Wasafi TV,” ameongeza.

“Kinachonichekesha na kunishangaza pale watu wanapoona nimemsupport akiwa na mafanikio, wanatak nianze kumkandia kitu ambacho hakiwezekani. Mimi Diamond ni mdogo wangu, wakati anatoka sikuwahi kuwa na bifu naye wala sikuwahi kukaa chini kumwambia ninatofauti naye, ni watu ambao wanataka kutuingiza katika tatizo mimi na Diamond,” amesisitiza.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW