BurudaniUncategorized

Msafiri aeleza mipango yake mwaka 2018

Muongozaji wa video nchini, Msafiri wa kampuni ya Kwetu Studios, ameeleza mipango ya ndoto zake katika mwaka huu wa 2018.

Akiongea katika kipindi cha Eight cha TVE, Msafiri amesema alikuwa na ndoto za kufanya kazi na wasanii wa nje katika mwaka huu ambapo tayari ameshapata dili kutoka kwa wasanii kumi mpaka sasa.

“Mwaka jana nilikuwa na dream kuwa mwaka huu lazima nifanye video na wasanii wa nje. Mpaka sasa kuna wasanii kama kumi wa nje ambao nataka nifanye nao,” amesema muongozaji huyo wa video.

Akiongea kuhusu watu wanavyozungumza video zake kukosa stori, Msafiri amesema hilo linatokana na tatizo kubwa la mashabiki wengi wamekuwa wakitengeneza script zao vichwani kabla ya video ya wimbo haijatoka.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents