Burudani

Msaga Sumu aja na ‘Mwanaume Mashine’

Mkali wa muziki wa Singeli nchini, Msaga Sumu amedondosha wimbo mpya ‘Mwanaume Mashine’ na kusema wimbo huo ni kwa ajili ya wanaume wote ambao wanajituma sana katika kazi.

Msaga Sumu

Akipiga stori na E Fm Radio, msanii huyo amewambia mashabiki wake wategemee video ya wimbo huo ndani ya wiki moja kwani sasa amejipanga kivinge ili kuwaletea burudani ya kukata na shoka ingawa upande wa management bado mambo hayajawa katika kiwango kile kinachotakiwa.

Katika upande mwingine msanii huyo amesema muziki wa singeli umemjengea heshima kubwa ingawa mwanzoni kuna watu walikuwa hawamuelewi lakini sasa kitu ambacho anaweza kujivunia.
“Muziki huu mimi nimeenda kumpa tuzo Isha Mashauzi mbele ya wageni na viongozi kibao, muziki huu pia umenitembeza nchi nzima,” amesema Msaga Sumu.

Msaga Sumu ameongeza kuwa kwa sasa ana uhakika muziki wake umeshika kasi mikoani na sio tena Dar es Salaam tu.

“Mimi namshukru Mungu nimetembea mikoa mingi mara baada tu ya kurudi kampeni, nimetembea sana kufanya show ila kuna utofauti. Kinachotukwamisha ni mipango, yaani kuwa na watu strong wa kukusimamia, sasa sisi mara nyingi unatakuta hatuna njia,” amesema.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents