Burudani

Miss Tanzania: Nilichopewa nimeshukuru, sijali watu wanachosema

Baada ya maneno kuwa mengi mtandaoni kuhusu gari alilokabidhiwa Miss Tanzania 2016/7, Diana Edward, mrembo huyo amefunguka na kusema yeye amefundishwa kushukuru, hivyo hana kipingamizi huhusu zawadi hiyo.

Diana Edward

Diana amesema hashangai watu kuongea hovyo kwa sababu hakunaga binadamu anayekubali kitu, ila yeye anachoangalia ni uwezo wao umefikia hapo wa kumpa hiyo zawadi hawezi akawalazimisha.

Gari alilokabidhiwa Diana jana

“Kwa hiyo zawadi nimeipokea, nawashukuru kamati, wazamini na watu wote waliosaidia hadi nikapata gari. Mimi sijui wanachokiongea ila situation ndiyo hiyo, nimeitwa nikaambiwa gari lako ndio hili nikalipokea kwa mikono miwili na shukrani.

“ Me I don’t care what people say, maneno yapo lakini siwezi kusikiliza nishindwe kuendelea na maisha mengine, wamenipa walichoweza kwa sababu wamehustler kutafuta hilo gari, watu hawawezi kujua kwa sababu wao wapo kwenye social media,” amesema Diana kwenye Leo Tena.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents