Msako wa Machangu wapamba moto

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni linawashikiliwa wasichana 12 kwa tuhuma za kukutwa wakijihusisha na biashara ya kuuza miili yao ( changudoa).

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni linawashikiliwa wasichana 12 kwa tuhuma za kukutwa wakijihusisha na biashara ya kuuza miili yao wajulikanao kama changudoa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Kanda Maalum Dar es Salaam, Marck Kalunguyeye amesema kuwa tukio hilo limetokea leo saa alfajiri, katika maeneo mbalimbali ya Kinondoni.

Amesema watuhumiwa hao (ambao hakutaka kuwataja majina yao), watafikishwa mahakamani leo.

Nao, wakazi 9 wa Ilala wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kukutwa na bangi pamoja na pombe haramu ya gongo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Kanda Maalum Dar es Salaam, Faustine Shilogile amesema kuwa watuhumiwa hao walinaswa jana saa 4 asubuhi, Mnyamani na Buguruni Madenge.

Watuhumiwa hao walinaswa wakiwa na bangi gramu 100 pamoja na pombe haramu ya gongo lita tano. Watuhumiwa hao wametajwa kuwa ni Said Abdalah (31), Abdalah Fikiri (30), Hassan Amir (32), Zainab Juma (30), Riziki Omary (26), pamoja na wenzao wanne.

Pia, wakazi wanne wa jijini wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kukutwa na puri moja ya bangi na gongo lita moja. Watuhumiwa hao walinaswa jana saa 3 asubuhi, Feri ambao nao ni Abdul Hemed (18), Dadi Said (32), Salum Ahmed (25) na Juma Abdalah (25). Watuhumiwa watafikishwa mahakamani leo.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents