Msanii Beka The Boy wa Kenya arudisha mkono kwa jamii

Ni mmoja kati ya wasanii wachache wanao kumbuka kule walipotoka. Beka The Boy ambae anatamba na kibao chake kipya kinachofahamika kama Zare, kupitia uongozi wake wa “Double B Production” chini ya usimamizi wake Francesca wamekua mashinani kwa majuma mawili mtawalia kutafuta vipaji ama talanta tofauti kwa vijana hususani kwenye soka.

Hatimae shuhughuli hii ilifikia kikomo ambapo msanii Beka The Boy aliifunga kwa kutoa burudani la kukata na shoka, kwenye eneo bunge la Magarini jimbo la Kilifili.

Tamasha hili lilihudhuriwa na mashabiki zaidi ya 2000, na washindi wa pambano zima la soka lililo dhaminiwa na Double B Production ambayo ndio msingi unaomshikilia Beka, uliweza kuwakabidhini washindi tuzo mbalimbali ili kuwatia moyo kua talanta inalipa. Chini ni link ya YouTube ikionyesha jinsi mambo yalivyokua.

Kuangalia video ya Show yake bofya HAPA

Imeandikwa na muandishi Changez Ndzai- Kenya

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW