Msanii Diamond Aweka Historia

Msanii chipukizi ambaye amekuja juu kwa kasi ya ajabu Diamond Jana usiku aliweza kuwa msanii wa kwanza chipukizi kupata tunzo tatu katika sherehe za kuwatunuku wasanii zinazokwenda kwa jina Tanzania Music Awards 2010, ambazo zinadhaminiwa na Kampuni ya Bia ya TBL kupitia kinywaji chake Kilimanjaro Lager.

Msanii huyo ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake cha “Mbagala” aliweza kufunika wasanii wakongwe baada ya kuchukua tunzo katika kipengele cha “Wimbo Bora R&B – kwa wimbo “Kamwambie“, Msanii bora anayechipukia na tunzo ya mwishoni katika wimbo Bora wa mwaka ambapo nyimbo Kamwambie ilichukua tena.

Katika sherehe hizo za utoaji wa tunzo za Muziki Tanzania makundi ya African stars wana twanga na kupepeta pamoja na kundi la Taarab la Jahazi Modern ziliweza kupata Tunzo mbili kila moja hali inayo onyesha ukomavu katika makundi yao ya ushindani kimuziki.

Sherehe hizo ambazo zilikuwa ni za mwaliko tu zikihusisha wadau mbali mbali wa muziki, burudani pamoja na marafiki wa kibiashara wa kampuni ya bia Tanzania ilianza mida ya saa 4 kamili na kuchukua takriban masaa mawili na dakika 40.

Washindi wengine waliopata tunzo ni pamoja na

Lady jaydee- mwimbaji bora wa Kike.

Banana Zorro- mwimbaji bora wa Kiume.

Nikipata nauli – Mrisho mpoto- wimbo bora wa asili ya kitanzania.

Stimu zimelipiwa- Joe Makini- wimbo bora wa Hip hop.

Leo (Reggae Remix)-A.Y- wimbo bora wa Reggae.

Mungu yuko Bize- Bwana Misosi- wimbo bora wa Ragga

Khalid Chokoraa-Rappa bora wa mwaka (Bendi)

Chidi Benz- Msanii bora wa Hip hop.

Haturudi nyuma- Kidumu Ft Juliana- wimbo bora wa Afrika Mashariki.

Mzee Yusuph- Mtunzi bora wa Nyimbo.

Lamar-Mtayarishaji bora wa nyimbo.

Problem- Cpwaa- Video bora ya muziki ya mwaka.

Pii pii- Marlaw- wimbo bora wa Afro Pop.

Nipigie-AT ft Stara Thomas-wimbo bora wa kushirikiana.

Sherehe hizo zilipambwa na burudani ya kupambana na shoka ambako THT, Twanga Pepeta, mzee yusuph, Joe Makini, Mwasiti, Marlaw, Ali Kiba, Banana zilihudhuriwa na msanii mwenye asili ya jamaica na anayeishi jijini Miami ambaye alikabidhi tuzoya wimbo bora wa Reggae Mungu yuko bize kwa bwana misosi.

Msanii huyo toka Jamaica anatarajiwa kutumbuiza jioni ya leo Diamond Jubilee Hall

Chini ni picha za sherehe hizo.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW