Habari

Msanii Jebby azikwa, wasanii wachanga Tsh. 550,000

Msanii wa Bongo Fleva, Jebby amezikwa katika makaburi ya Mailimbili mjini Dodoma.

Jebby ambaye amewahi kufanya vizuri na wimbo wake wa ‘Swahiba’ alifariki dunia hapo jana April 22, 2018 mjini Dodoma alipokuwa akipatiwa matibabu.

Wapili kushoto ni msanii Suma G.

Kwa mujibu wa mdogo Jebby, Hamis Omary msanii huyo hakubahatika kuwa na mke wala mtoto, pia kuna nyimbo zaidi ya nne alirekodi ambazo zipo tayari ila hazijatoka.

Professor Jay ni miongoni mwa wasanii waliohudhuria katika msiba huo ambapo amekabidhi Tsh. 550,000 zilizochangwa na wasanii kwa ajili ya msiba huo, msanii mwingine aliyehudhuria ni pamoja na Suma G.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents