Burudani

Msanii mkongwe wa Marekani afariki dunia

Msanii mkongwe wa muziki kutoka Marekani, Thomas Earl Petty amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 66.

Meneja wa zamani wa msanii huyo, Tony Dimitriades amethibitisha kutokea kwa kifo hicho katika hospitali ya UCLA Medical Center huko mjini California.

Inadaiwa kuwa siku ya Jumapili iliyopita msanii huyo alianguka ghafla akiwa nyumbani kwake kutokana na maradhi ya moyo na alikimbizwa hospitalini hapo ambapo hali yake ilioekana kuwa mbaya zaidi.

Petty atakumbukwa kwa ngoma zake kali ikiwemo ‘American Girl’, ‘I won’t back down’ na nyingine. Hii hapa chini ni moja ya ngoma ambazo msanii huyo aliiachia enzi za uhai wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents