Burudani

Msechu aomba radhi kuvaa mlegezo

peter_msechu_radhi
Mwanamuziki Peter Msechu amesema leo ndiyo ameanza kuachia video na Audio ya wimbo wake yeye na Kidumu wa Relax. amesema video hiyo ambayo itakuwa babu kubwa anaamini itamuweka sehemu mzuri. pia mkali huyo kutoka Bss na Tusker


Project Fame amesema anawaomba RADHI ndugu , jamaa, marafiki na mashabiki wake wote, baada ya kumchukulia vibaya siku ya tamasha la Bongo Star Search second chance Final kwa jinsi alivyovaa mlegezo.

Msechu anasema halikuwa lengo lake kuvaa hivyo ambapo kulimpelekea kuonyesha nguo yake ya ndani na baadhi ya sehemu ya mwili. Msechu anasimulia kw kusema siku hiyo ya fainali ya tamasha hilo, alijipanga na kununua pamba mpya kwaajili ya kushine, jambo ambalo alifanikiwa.

Anasema muda wa kuwasili kwenye tamasha ulifika akiwa amezitinga nguo hizo ndipo akagundua nguo moja ya ndani aliyovaa iliwa imeachia ghafla, katika misheshe za hapa na pale na hatmaye ikawa inashuka chini. anasema  alifikiria kuivua lakini muda ulikuwa umeshaisha wa yeye kupanda jukwaani.

Msechu anasema akaona haina jinsi ni bora kwenda kujaribu kuona kama angeweza kufanya shoo huku akiizuia isije ikamuumbua, ndipo akajikuta akikosa amani na kwa kushuka nguo hiyo na jinzi, na kumtengenezea bonge la mlegezo  jambo ambalo hakuwa kulizuia.

Kutokana na jambo hilo, anawaomba radhi mashabiki wake, ambao hawakupendezewa na kitendo kile, kwani hata yeye kilimuudhunisha sana, “Sikutarajia kama ingekuwa vile, hata nyumbani walipoiona ile show, walisema nimebadilika kwa kuvaa milegezo” alisema.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents